Mwenyekiti CHADEMA kijiji cha Ivalalila Makete Godfrey Mahenge akizungumza mara baada ya kutoka jela.

======
Na Edwin Moshi, Michuzi Media, Makete

Jeshi la polisi nchini limeaswa kutenda kazi kwa haki bila kushurutishwa na mtu yeyote kwani lisipofanya hivyo haki haitatendeka kwa kila raia kama katiba inavyosema

Rai hiyo imetolewa hii leo na mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Ivalalila wilayani hapo waliojitokeza kumpokea mwenyekiti wa CHADEMA kijijini hapo aliyekuwa gerezani mara baada ya kuachiwa huru
 
"jeshi la polisi ni zuri sana pale litakaposimamia haki, lakini wanapokwenda kinyume kwa kweli wanageuka mwiba mchungu kwa wananchi" alisema Mkakanze 

Mkakanze amesema hukumu iliyotolewa na mahakama ya mwanzo makete mjini Juni 28 mwaka huu dhidi ya mwenyekiti huyo imeonekana kuwa na mapungufu mengi ambayo amesema atayataja katika mkutano wa hadhara utakaofanyika muda wowote kuanzia sasa, hivyo ndiyo maana wameibuka kidedea katika rufaa waliyokata

Amesema wao kama chama hawatakatishwa tamaa na mambo kama hayo na badala yake wataendelea kupigania haki za wananchi pale wanapoonewa na ikibidi hata kupoteza maisha wakati wakipigania haki zao

"Chadema sisi si watu wa vurugu, lakini sisi tunasimamia haki na maendeleo ya wananchi bila kujali  itikadi za vyama, hata yeyote tupo pamoja nae kama anatenda haki na kile anachotakiwa kuwafanyia wananchi lakini anapokwenda kinyume sisi hatutakubali na badala yake tutapambana mpaka kieleweke" alisema Mkakanze

Naye mwenyekiti wa CHADEMA kijiji cha Ivalalila ambaye alikuwa gerezani Bw Godfrey Mahenge amesema hana cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu na wananchi wa kijiji hicho ambao walikuwa naye pamoja tangu wakati wa kesi hadi gerezani na kusema kwa sasa ametoka na wembe ni ule ule wa kupigania haki za wananchi wake

Amesema kwa sasa hana mengi ya kuongea zaidi atakuja kuzungumza kwenye mkutano wa hadhara ambao utaandaliwa kwa ajili ya wananchi hao ambapo anatarajia kueleza yote yaliyomkuta ili wananchi wake wajue, huku akitoa rai kwa waandishi wa habari kutangazia umma kuwa hivi sasa yuko huru na kesi zote ameshinda

"Nawaomba waandishi wa habari kama mlivyotangaza wakati nafungwa naomba mtangaze pia na jinsi nilivyoshinda rufaa na kuwa huru" alisema Mahenge

Mnamo Juni 28 mwaka huu mahakama ya mwanzo makete mjini ilimtia hatiani kwa kosa la kutukana polisi hivyo kuhukumiwa kifungo cha miezi 9 gerezani hali iliyomlazimu kukata rufaa na kushinda rufaa hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. pole sana m-kiti kwani wewe ni mpiganaji wa ukweli umedhiirisha kuwa huko tayari kwenda jela kupigania uhuru na demkorasia ndani ya nchi hii pole sana kamanda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...