
DIWANI ATHUMANI – ACP
--

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAWATAKA MASHABIKI NA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU WAACHE VITENDO VYA KUFANYA VURUGU KATIKA MICHEZO ITAKAYOKUWA IKIFANYIKA KATIKA UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE NA MKOA KWA UJUMLA, KWANI VURUGU HIZO ZITASABABISHA MICHEZO HIYO KUHAMISHIWA SEHEMU NYINGINE NA WAPENZI KUKOSA BURUDANI PIA WANANCHI KUKOSA KIPATO, HIVYO KUUTANGAZA MKOA WETU VIBAYA.
VURUGU ZILIZOTOKEA JUMAMOSI TAREHE 14/09/2013 KWA MASHABIKI KULISHAMBULIA GARI LA VIONGOZI WA TIMU YA YANGA LILILOKUWA LIMEPAKI NJE YA UWANJA PIA KULISHAMBULIA KWA MAWE GARI LILILOKUWA LIMEBEBA WACHEZAJI WA TIMU YA YANGA NA KUHARIBU KIOO CHA MLANGO WA DEREVA NA KUFANYA MAANDAMANO AMBAYO YAMESABABISHA USUMBUFU KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA SI CHA KIUNGWANA NA KISIJIRUDIE TENA KATIKA MICHEZO MINGINE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA HAKURIDHISHWA NA VITENDO HIVYO NA KUWATAKA MASHABIKI NA WAPENZI WA MPIRA WA MIGUU KUWABAINI NA KUWATAMBUA WALE WOTE WATAKAOFANYA VURUGU NA KULIJULISHA JESHI LA POLISI.
AIDHA JESHI LA POLISI HALITAVUMILIA VITENDO HIVYO NA KWA YEYOTE ATAKAYE/WATAKAO BAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA ZIDI YAKE/YAO.
Signed by:
P.A MHAKO – ASP
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...