KAULI ZA KISIASA
 Hivi karibuni mnamo tarehe 21/09/2013 vyama vya siasa kadhaa vilifanya mkutano wa hadhara katika Viwanja vya Jangwani, Pamoja na mambo mengine yaliyo zungumzwa, mimi kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nimestushwa na baadhi ya ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi. Ambao unaweza kuleta madhara kwa jamii, hususan wanawake, watoto, wazee, walemavu n.k.
                                    
Kwanza, Kauli ya Mhe. Lipumba
Mheshimiwa huyu kati ya maneno yote aliyoyasema pale Jangwani, nadhani jamii inahitaji kutafakari na kuhoji; maana ya kauli yake aliposema, “Vijana msikubali wakati wa kufanya mazoezi umefika” Tujiulize, Je, ni mazoezi ya aina gani? Yanafanyikia wapi? Yanalenga kufanya nini? Lakini mwisho wa yote ni muhimu Watanzania wakajikumbusha mwenendo wa siku za nyuma za hao wanaoitwa vijana wake!

Wito wangu kwa vijana wasikubali kutumiwa katika mambo yanayo wahatarisha wao na jamii kwa ujumla, kwani hayana tija. Wananchi kumbukeni kuwa yanapotokea matatizo, akina mama ndio walezi wa majeruhi, wagonjwa na pia walezi wa watoto wa walioathirika.

Pili, Kauli ya Mhe. Mbowe
Mheshimiwa huyu kati ya maneno yote aliyoyasema, nilipatwa na butwaa kwa kauli yake aliposema:- “Siku ya tarehe 10/10/2013 ni Siku Maalum ya Kitaifa ya “Civil Disobedience”. Hii ni kauli hatari, yenye kuashiria uwepo wa njama mbaya za kuwashawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria mkononi, kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu.

Tujiulize “Siku Maalum ya Kitaifa ya Civil Disobedience” maana yake nini? Kwa Kiswahili maana yake ni Siku Maalum yaKitaifa ya Jamii Kutotii, kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa. Hayo yakitokea itakuwa ni Siku ya Maangamizi. JAMII KUTOTII ni utovu wa Nidhamu, ambao husababisha Uvunjaji wa Sheria na kuhamasisha kujenga Mazingira ya Vurugu.

Kwa nafasi yangu kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nasema hii ni hatari. Na athari zake naziona kubwa kwa wanawake, watoto, walemavu na wazee.

Tatu, Kauli ya Mhe. Mbatia
Mheshimiwa huyu kati ya maneno yote aliyoyasema, nadhani jamii inahitaji kutafakari na kumpongeza kwa kauli yake aliposema:- Bado anaamini kwamba “Kuna fursa ya kukaa katika round table na kuyazungumza”. Hii kauli ni ya kizalendo na ya kiungwana. Nampongeza sana. Inavyoonekana, Mhe. Mbatia ni mtu mwenye kutambua kwamba ana dhamana ya kuilinda familia yake na jamii ya Watanzania kwa ujumla.

Tahadhari ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii
Mwenendo wa kauli hizi, si mzuri kwa maendeleo na ustawi wa jamii yetu kijamii na kiuchumi. Hii ina maana siku hiyo ya Civil Disobedience, Mama Lishe na Wajasiriamali wengine hawatofanya biashara zao, watoto wetu hawatoenda shule na huduma nyingine za kijamii zitakwama wakati wao wakitekeleza mipango waliyopanga kwa tarehe hiyo.

Amani na usalama ni mtaji wa maendeleo
Kama jamii tunapaswa kutambua kwamba amani na usalama, ndio mtaji namba moja wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Ustawi wetu kama jamii ya Watanzania au kama familia au mtu mmoja mmoja unahitaji uwepo wa amani, utulivu na usalama. Kwa sababu kunapotokea vurugu/Civil Disobedience wanaoathirika zaidi ni wanawake, watoto, wazee na walemavu.Leo nimeona niongelee hili ambalo linawagusa wadau wangu moja kwa moja ambao wapo chini ya Wizara yangu.
Asanteni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwani serikali hamna sharia ya kuwashitaki kwa lengo la kutaka kuvuruga amani? Lazima kuwe na sharia ya kukataza watu ambao ni viongozi ktk vyama kuchochea vurugu ktk nchi yetu hata viongozi wa dini.Na kama hamna hiyo sharia basi zitungwe hizo sharia.Hii hinaonyesha hawa viongozi wa upinzani wana uchu sana kuongoza nchi, JIULIZE NI KWANINI?Kama kweli ni wazalendo na wanauchungu na Tanzania kwanini wasifanye mikutano ya kuchangisha hela za kujenga Hospital,Mashule.barabara za vijijini huko walipochaguliwa,Kwanza huyo Mbowe ktk wilaya yake kunamatatizo ya barabara ,hospital ,majambazi.maji ,umeme nk.especialy barabara za Mailisita hazipitiki makorongo kibao mpaka shule ya msingi ya Njoro majengo yana poromoka pia shule ya Mailisita ,kama kweli hanauchungu kwanini hasfanye harambee ya kuzikarabati hizo shule hanyeshe mfano.Mahakama ya hai ni aibu tupu.Next election sahau mailisita ni CCM TU.Hatutaki vurugu ktk nchi yetu siyo Disco

    ReplyDelete
  2. Hapa duniani kila mtu anatetea tumbo lake tu! iwe ni mrengo wa kushoto, kulia au kati wote wanafikiria matumbo yao na familia zao. Kilichobaki wewe MTU WA CHINI ufikirie namna ya kujikomboa wewe mwenyewe katika maisha yako, hakuna anayeweza kukusemea wewe kwa niaba yako au kufikiria kwa niaba yako, awe mpinzani au aliyeko madarakani kwani wote hawa ni WANASIASA.

    ReplyDelete
  3. Mbowe na Lipumba ni majanga ya Taifa letu. Wote tunaamini kwamba CCM kuna nyufa ambazo zinahitaji kuFanyiwa kazi na zinazotumiwa na wapinzani ila huwa hainiingii akilini kuwa waheshimiwa hawa wana uwezo wa kulinda amani yetu ya nchi.sawa mafisadi nao wanagharimu jamii ila jamii yetu inabidi itafakari sana juu ya hawa watu sina imani kuwa wanaweza kulinda amani sawasawa na CCM WALIOWAFIKISHA HAPO WALIPO .kamwe hatutavumilia wachumia tumbo wachache wa kuchezea tunu yetu ya Tanzania hata kwa gharama ya ufisadi tuko tayari.

    Mdau UK-sina chama

    ReplyDelete
  4. Taarifa hii iwafikie Watanzania wooote. Wanasiasa msiichezee amani ambayo ni tunu yetu. Wizara nyingine jeeee? Mmeona yaliyosemwa yote ni sawa? Mtajibu lini? Mungu tuepushe na balaa Tanzania.

    ReplyDelete
  5. Haya Asante tumekusikia lakini ungejaribu pia kutega sikio na kunukuu kauli tata za upande wa pili pia maana zipo na tunazisikia pia. Kwa kuleta taarifa za upande mmoja sidhani kama yaonesha kweli kujali au msaada kwa jamii bali ni funzo baya.Mwisho wa siku maamuzi yatabaki kwetu sisi wananchi wenyewe msidhani kua hatuoni au hatujui kinachoendelea.

    ReplyDelete
  6. Mm namuomba rais kikwete atumie busara kuiponya nchi yetu coz hizi kauli za hawa viongozi ni nzito na ni hatari sn,nakuomba kikwete uwasikilize hawa watu kisha uwaulize wapi tumekosea? Ili palekebishwe haraka sn,hii katiba ni yetu wote watanzania tukifanya masihara tutakuja kujuta na tutachekwa na kila taifa,jamani ndugu zangu watanzania katiba ci CHAI ikimwagika inawezekana kupika nyingine but katiba tukiikosea ndio tumeikosea na mwenye masho haambiwi ona tuungane tupendane na tuilinde nchi yetu na amani yetu, ni hayo tu kwaleo,NAITWA mdudu kakakuona napatikana UINGEREZA au UK,mkaekwa AMANI wote huko nyumbani nawapendeni pia wote.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Mh. Simba tunakuunga mkono na hao wahalifu hatuta wapa nafasi ng'odo.

    ReplyDelete
  8. HONGERA MAMA SOFIA SIMBA, HAO WANAOJIITA VIONGOZI WA WATU WAMEFILISIKA HOJA SASA WANATAKA KUTUMIA NGUVU. SISI HATUNA NAFASI HIYO, TUNAYOTAKA MAENDELEO MAJI, ELIMU, BIASHARA. TOKA WAMEINGIA CHADEMA BUNGENI FUJO TUPU!! MBONA MIAKA YOOOTE YA VYAMA VINGI HATUJAONA NGUMI NA VITUKO BUNGENI? DEMOKRASIA DUNIANI KOTE NI BUNGENI SASA KAMA LIPUMBA KAMCHAGUA NANI? HAO KINA MBOWE NA TOTO TUNDU LISSU SI WAPO BUNGENI? KWA NINI HAWASEMEI BUNGENI???

    ReplyDelete
  9. CCM huwa inasahau HAKI ! siyo tu kuimba amani. Haki ya watu kutopata bugudha wakati wanatafuta kipato chao cha kila siku na kuwepo na mazingira ya upatikanaji kipato bila usumbufu, haki ya kua na soko la ushindani wa kweli sio wachache kuhodhi njia za upatikanaji vipato, haki mbele ya sheria (polisi,mahakama), Haki ya wananchi kupitia serikali yao kumiliki Gas % kubwa (kama Gulf states and nchi nyingine hata Uingereza ina shares kwenye Major companies) na pesa ziwekwe kwenye infrastructure projects na kurahisihsa jamii kufanya biashara na kusafiri na uwekezaji wa wananchi kwenye sekta za jamii utawezekana,Haki ni nyingi hizo ni baadhi tu. Hapo ndipo maneno yataisha ...Ya pande zote! Atakaeleta Haki ataleta Amani na maendeleo. Not vice versa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...