Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, leo amewasili nchini akitokea India alikokwenda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, Maalim Seif alipokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Abdallah Mwinyi Khamis.

Aidha mapokezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na viongozi pamoja na wafuasi wa Chama Cha Wananchi CUF, yaliambatana na shamra shamra mbali mbali za burudani.

Maalim Seif aliondoka nchini tarehe 24 mwezi uliopita kuelekea India kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake, utaratibu ambao umekuwa ukifanyika tangu alipofanyiwa upasuaji wa goti miaka mitatu iliyopita.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi Khamis pamoja na viongozi wengine, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbali mbali, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisawapungia mkono wananchi waliojitokeza kumpokea, wakati akiwasili nchini akitokea India kwa uchunguzi wa kawaida wa afya yake.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mama Awena Sinani Masoud (kulia), alionesha uso wa bashasha baada ya kuwasili nchini akitokea India. (picha na Salmin Said, OMKR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nafikiri matumizi ya neno kawaida siyo mazuri maana mheshimiwa kaenda India kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida kwanini isiwe ni hapa hapa, huu utakuwa ni uchuzi maalum. Tusitake kuwasingizia viongozi wanaenda india hata vijigonjwa vidogo vidogo kama ndiyo hivyo hospitali zetu zitaendelea kufa kwani wangalizi wake hata wakiwa na mafua wanaenda nje

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...