Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho  Kikwete amesema kwa sehemu kubwa utekelezaji wa maendeleo ya millenia umefanikiwa nchini mwake licha ya kwamba yako malengo ambayo bado hayajafanikiwa matahalani usafi wa mazingira na kuanisha mipango iliyopo katika kuyatimiza. 
 Katika mahojiano maaluma na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa Rais Kikwete amesema nchi zilizoendelea zimekuwa zikisita kutimiza lengo namba nane linalowataka watoe asilimia saba ya pato la taifa ambapo akitoa mfano kwa nchi kama Marekani amesema ni kiasi kikubwa na hivyo kutotomizwa jamabo ambalo kwa ujumla linachelewesha utekelezaji wa malengo hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ANGALIZO: NI 0.7% NA SI 7% KAMA MWANDISHI ALIVYOANDIKA. O.7% YA PATO LA TAIFA. MAANA YAKE NI KWAMBA KATIKA KILA DOLA MOJA YA KIMAREKANI WANAPASWA KUTOA SENTI 0.7 NA KAMA NI DOLA MIA MOJA WANAPASWA KUTOA SENTI 70 TU. UCHUMI WA MAREKANI KWA SASA UNA PATO LA TAIFA LA DOLA TRIONI 16.663. KWA HIYO WANAPASWA KUTOA KWA HESABU YA HARAKA WAMAREKANI WALIPASWA KUTOA DOLA BILIONI 116.641 KUSAIDIA KUTIMIZWA KWA MALENGO YA MILENIA KILA MWAKA. HAWAJAWAHI KUTOA HATA MOJA YA MIA YA PESA HIZO TOKEA 2001. KICHEKESHO NI KWAMBA HAO HAO WAMERAKANI NI NDIO WA KWANZA KUZIKABA KOO NCHI MASIKINI KUPITIA MIKOPO YENYE RIBA KUBWA YA IMF NA WORLD BANK. KIMSINGI HAWANA NIA YA KUONDOA UMASIKINI WA KUZISAIDIA KWA DHATI NCHI MASIKINI. SENTI 70 KWA DOLA MIA MOJA NI KITU GANI. KUTOA NI MOYO. NA MOYO HUO HAWANA.

    AMANI MILLANGA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...