-Na Freddy Macha
Mchoro wa shughuli uliobuniwa na Sara Abood.
Wabunifu mavazi wanne toka Tanzania walioshiriki maonesho ya mavazi Ubalozi wetu London
Jumamosi Septemba Saba wamechaguliwa kuingia dimba la kimataifa London Fashion Week,
Februari mwakani.
Wasanii hao waliopewa nafasi ya kujitangaza kupitia jitihada za Jumuiya ya Wanawake
Uingereza (TAWA) ukishirikiana na Ubalozi ni mseto wa wafanyabiashara wakongwe na vijana
wanaoanza fani hii ya urembo.
Mama Joyce Kallaghe, ni mtangazaji mzuri wa mavazi ya Kitanzania ughaibuni. Picha na
Felipe Camacho.
Akifungua shughuli hii, mkewe Balozi, Mama Joyce Kallaghe alikumbusha hii ni nafasi nzuri
kwetu.
“ London Fashion Week” ni tafrija maarufu inayofanyika sambamba Paris, New York, Milan
mwezi Februari na Septemba kila mwaka toka 1984. Mbali na msaada wa TAWA na Ubalozi,
mwekezaji mkuu wa shughuli hii ni British Council- shirika linaloendeleza vipaji nchi zaidi ya 100
duniani kwa miaka 75 sasa.
Mada ya maonesho iliitwa “Fahari Passion 2013” na mchoro wake uliobuniwa na Bi. Sara
Abood unaonyesha uso wa mwanamke na rangi za bendera ya taifa.
Khanga inavyojigamba na kupendeza. Picha na Abubakar Faraji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...