Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (mwenye kipaza sauti) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Wanafunzi wa Vyo mbali mbali Mkoani Tabora,waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Ukumbi wa Chuo cha Utumishi,Mkoani Tabora leo Septemba 13,2013.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (katikati) akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Tabora,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Tabora Mjini,mchana wa leo Septemba 13,2013.
Msafara wa Pikipiki (maarufu kama Boda Boda) Mkoani Tabora ukiwa barabarani wakati wa kumpokea Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipokuwa akiwasili Mkoani Tabora leo,ambapo alitembelea Ofisi za Chama cha Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora.
Mwenyekiti wa Chama Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoani Tabora,Waziri Kipusi (kushoto) akisoma taarifa fupi mbele ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa juu ya mwenyendo wa Chama hicho pamoja na malengo yake.ambapo Mh. Lowassa ameahidi kuwapatia pikipiki tatu,ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwenye Chama hicho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache kwenye mkutano wake ya Waendesha Boda Boda wa Mkoa wa Tabora.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...