Spika wa Bunge la Seychelles,Mhe Dr.Patrick Herminie (kulia) akiwa na Katibu wa Bunge la nchi hiyo,Bi.Azarel Ernesta wakipata maelezo kuhusu Maandalizi ya mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola kwa Bara la Afrika.Jumla ya Maspika toka nchi 19 za Afrika watahudhuria mkutano huo.Maafisa wa Sekretarieti watakaohudumia mkutano huo ni Ndugu Demetrius Mgalami,Katibu Msaidizi wa CPA Afrika(wa kwanza kushoto),Ndugu Saidi Yakubu,Mratibu wa Chama hicho bars Afrika(wa pili kushoto) na Ndugu Ephraim Jane toka Bunge la Namibia.Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola kwa Bara la Afrika kinaundwa na nchi 19 ambazo ni Botswana,Cameroon,The Gambia,Ghana,Kenya,Lesotho,Namibia,Nigeria,Malawi,Msumbiji,Mauritius,Rwanda,Seychelles,Afrika Kusini,Swaziland,Sierra Leone,Tanzania,Uganda na Zambia.Makao Makuu ya Chama hicho yapo katika Bunge la Tanzania ingawa pia maafisa wengine huombwa toka Mabunge mengine kulingana na mahitaji
Picha ya pamoja baina ya Spika wa Bunge la Seychelles Mhe.Dr Patrick Herminie na Wajumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola Mara baada ya kumalizika kwa kikao cha maandalizi.Kikao hicho kilifanyika katika Bunge la Seychelles mjini Mahe. Pichani toka kushoto ni Bi Azarel Ernesta,Katibu wa Bunge la nchi hiyo,Nd.Ephraim Jane,Afisa wa Sekretarieti toka Namibia,Nd.Demetrius Mgalami,Katibu Msaidizi wa CPA barani Afrika, Spika Herminie,Nd.Saidi Yakubu,Mratibu wa CPA Barani Afrika  na Nd.Molathe Moshifane,Afisa wa Sekretarieti toka Afrika Kusini. Picha kwa hisani ya Ofisi ya Bunge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. kwa hapa bongo ukiitishwa mkutano wa watu warefu Saidi unaweza kuingia hata kama ni kwa kujiiba.

    lakini hiyo njemba pembeni yako imefanya uonekane bado unahitaji kurefuka.

    having said that, kazi yako nzuri inaonekana hata kwetu tulio nje ya bunge - safi sana, good ambassador.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...