Mrembo Severina Lwinga juzi alifanikiwa kuwa mrembo wa tano kuingia nusu fainali ya shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 baada ya kutwaa taji la Miss Personality 2013. Mshindi wa taji hilo anapatikana kwa kupigigiwa kura na warembo wenzake.
Severina ameungana na Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo kuingia katika nusu fainali ya Miss Tanzania ambayo itafanyika Jumamosi hii ukumbi wa Mlimani City. Shindano hilo lilifanyika Mgahawa wa AK'S ulipo mtaa wa Samora.
 Warembo walioingia tano bora ya Miss Personality 2013 shindano lililofanyika katika magahawa wa AK'S uliopo Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
Warembo watano ambao wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya Redd’s Miss Tanzania 2013 wakiwa katika picha ya pamoja mara jana. Kutoka kushoto  ni Miss Tanzania Photogenic 2013, Happiness Watimanywa, Miss Tanzania Talent 2013, Prisca Clement, Miss Tanzania Personality, Severina Lwinga, Miss Tanzania Top Model 2013, Narietha Boniface na Miss Tanzania Sports Woman, Clara Bayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

 1. Na wenye Mimba wanaruhusiwa?

  ReplyDelete
 2. hata mimi nimeshangaa ni nini hicho kilichojitokeza hapo mbele??

  ReplyDelete
 3. no, just a big breakfast! it is not mimba. Unasema mimba kwani wee ni daktari?

  ReplyDelete
 4. hahaha eti big breakfast!!!! duh ama kweli kuishi kwingi.....

  Binti kitumbo anacho na sio cha big breakfast, ni mimba au sio mimba anaejua ni yeye mwenyewe FACT

  ReplyDelete
 5. Leave her alone plz, hiyo ni nundu tu

  ReplyDelete
 6. Usifanye mchezo na misosi ya bureee

  ReplyDelete
 7. Hatutashinda hata siku moja. Yaani mrembo amefumuka tumbo hivyo ndio tunakwenda mshindanisha? Nakumbuka kuna mwaka tulipeleka mwenye mwanya!!

  ReplyDelete
 8. sio mimba jamani, hizi chipsi sio zenyewe. Kama hupigi sit ups matokeo yake ndio haya. Ila nywele mmeona?

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...