Wachezaji wa Simba na Ruvu JKT wakisalimiana kabla ya pambano lao la Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba imeshinda 2-0. (Picha na Francis Dande)
 Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki akimiliki mpira huku akizongwana na wachezaji wa JKT Ruvu, Nashon Naftali (kulia) na Emmanuel Pius wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa.
 Kizaazaa
 Mwamuzi wa mchezo huo, A. Kayombo kutoka Rukwa akiwatuliza wachezaji wa JKT Ruvu baada ya kuilalamikia pelnati waliopata Simba. 
 Mnazi wa Simba akifurahia matokeo ya mechi ya leo.
 Joseph Owino akichuana na Mshambuliaji wa JKT Ruvu, Amos Mgisa.
Mshambuliaji wa Simba, Haruna Chanongo akichuana na beki wa JKT Ruvu, Stanley Nkomola. Picha na Francis Dande

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongera sana vijana wa msimbazi! 2-0 .... aah huu si ushindi wa kubahatisha inaonekana mlikuwa mnajua mnachotakiwa kufanya; nadhani ni heshima pia kwa kocha mzalendo, Abdallah Kibaden "King Kibaden" congratulations!

    ReplyDelete
  2. Vijana wa msimbazi huwa mnaazaga ligi kwa vishindo na makelele mengi.Sisi wana Yanga aka watoto wa Jangwani tumetulia tunasubiri mwisho wa ligi tuu. Michuzi usibanie hii comment maana wewe ni Simba damu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...