![]() |
Msemaji wa Polisi SSP ADVERA SENSO |
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika katika utekelezaji wa maazimio ya kikao cha 21 cha wakuu wa polisi Afrika kilichofanyika Gaborone Botswana mwaka 2011, katika kuzuia na kutanzua makosa yanayovuka mipaka (Transitional Cross Border crimes).
Hayo yameelezwa katika kikao cha 22 cha wakuu wa polisi kutoka nchi za Afrika (Interpol African Reginal Conference) kilichofanyika nchini Algeria kuanzia tarehe 10-12 Septemba, 2013.
Miongoni mwa makosa yaliyofanikiwa kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa na Jeshi la Polisi kupitia interpol Tanzania na kuiletea sifa nchi ya Tanzania, ambayo yamekuwa yakivuka mipaka ni pamoja na ugaidi, uharamia, usafirishaji haramu wa binadamu, uzagaaji wa silaha ndogondogo, usafirishaji wa madawa ya kulevya na uingizaji wa dawa bandia.
Mbali na azimio hilo, maazimio mengine yaliyokuwa yameafikiwa kutekelezwa yalikuwa ni kuhakikisha kila nchi mwanachama wa interpol anajiunga katika mtambo wa mawasiliano wa interpol, kushiriki oparesheni za pamoja zinazoandaliwa na nchi wanachama na kushiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa wa polisi kwa lengo la kupambana na uhalifu, ambayo pia Jeshi la Polisi Tanzania limefanikiwa kuyatekeleza.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Nfikiri madawa ya kulevya hayakuhusishwa katika huo mchakato, vinginevyo tungekuwa wa kwanza kutoka mwisho.
ReplyDeleteNaona Kamzuzu poa.
ReplyDeleteTatizo letu huwa hodari kufanya usanii,ktk madawa ya kulevya,hapo hapana. Watz sasa tunadhalilishwa duniani ktk security checks,hawaangalii mzee/kijana,unatomaswatomaswa mwili wote kama Tonge la ugali,pindi uoneshapo tz passport,hii ni hali mbaya sana. Maofisa wanatakiwa kutoka nje ya nchi,wajionee wenyewe,nina hakika wanapewa typed report,hii ni kimdhalilisha mtoa report.
ReplyDelete