Zuberi Mussa  katika muonekano wa picha tofauti 
tofauti nje ya Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mazinde.

Zuberi Mussa (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mwandishi Dotto Mwaibale (kushoto), Mashaka Kibaya (kulia) wote wa Gazeti la Jambo Leo na Mashaka Mhando wa Gazeti la Majira mkoani Tanga, walipokwenda kumjulia hali kijjiini kwao.

Na Dotto Mwaibale, Tanga

Zuberi Mussa ambaye ni mpiga picha mkongwe katika vyombo mbalimbali vya habari nchini ambaye kwa sasa anafanyakazi Kampuni ya New Habari ni mgonjwa anayehitaji msaada wa hali na mali.

Kikubwa kinacho msumbua mwandishi mwenzetu huyu ni ugonjwa ambao bado haujafahamika ambapo kwa mtu anayemfahamu ni rahisi kumgundua kuwa ana matatizo ya kiafya kwani katika kila sentesi yake ya pili na ya tatu wakati wa kuongea naye hautaelewana naye kutokana na matamshi yake ambayo hayafahamiki yanayoonesha  kama mtu aliyechanganyikiwa.

Kutokana na kukosekana kwa fedha za kumsaidia katika matibabu hasa Hospitalini, Zuberi Mussa amelazimika kwenda kupata matibabu yake kwa waganga wa jadi.

Wakati Zuberi akiwa kijijini kwao Kata ya Mazinde wilayani Korogwe mkoani Tanga bila ya kuwa na msaada wowote mke wa mwenzetu huyo aitwaye Rehema Amir kwa kipindi cha mwaka mzima yupo hoi kitandani kutokana na maradhi ya kupooza yaliyompata mwanzoni mwa mwaka jana akiwa jijini Dar es Salaam, hawezi kufanya chochote ikiwa ni pamoja na kuongea hakika inaumiza na kusikitisha.

Ndugu wanahabari kila mmoja wetu kwa imani yake na utamaduni tulionao wa kusaidiana tujitokeze kumsaidia mwenzetu huyu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

Binafsi nilipofika kumuona kwa mara ya kwanza wiki iliyopita nilishitushwa na hali aliyokuwa nayo ingawa kaka yake aitwaye Waziri Mussa anayemuuguza alidai kuwa alikuwa amepata nafuu.

Zuberi alifika katika eneo nililokuwepo akiwa katika hali ambayo si ya kawaida zaidi ya kusalimiana na kunitambua mengine yote nilioongea naye hatukuweza kuelewana. Kwa mtu yeyote atakayependa kumsaidia Zuberi pamoja na mke wake kipenzi  Rehema Amir anaweza kuwasiliana na Dotto Mwaibale kwa namba 0712-727062 ambaye atakuunganisha na kaka yake.

Ndugu wanahabari wenzangu  na mtu mmoja mmoja, Taasisi yoyote, shirika lolote, Mfuko wa Taifa wa  Bima ya Afya, Wafanyabiashara, Makampuni mbalimbali na vyama vya michezo  hima tujitoe kimasomaso kumsaidia mpiga naji mwenzetu Zuberi Mussa na mke wake waondoke katika matibabu ya jadi wanayopata kwa waganga wa kienyeji badala yake wapelekwe hospitali kwa uchunguzi zaidi wa afya zao kwani kutoa ni moyo na si utajiri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. ushauri tu jaribuni kuangalia kwenye mtandao maana siku hizi magonja mengi yapo expalained kwenye mitandao hii ulivyosema kwenye report inaonyesha kama dementia ni ugonjwa wa kusahau ambao unakuja kwa aina nyingi. Huu ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  2. Huo ugonjwa utakuwa unaitwa TROUT SYNDROME kwa jinsi ya maelezo yako ndugu mwandishi. Huu ugonjwa hupo kuna dada mmoja mwingereza yeye akiwa anaongea kuna sauti inatoka ya neno biscuits yaani kama vile background voice inashangaza sana na mwingine yeye mpaka kaacha kazi maana kila maneno matatu lazima tusi linatoka tena kwasautifulani ya ajabu sana.uki GOOGLE TROUT SYNDROME NA CHEKI KWENYE YOUTUBE majibu yatapatikana . Tiba huwa hamna. Hapa UK wenye hillo tatizo wanajumuiya yao angalau wenyewe kwa wenyewe wanafarijiana. Sio uchawi wala nini huo ugonjwa upo.

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni DEMENTIA ambayo baadaye inakuwa ALZHEIMER

    ReplyDelete
  4. TOURETTE SYNDROME,
    hata mimi nnayo lakini iko chini sana naweza kubana mdomo nsitamke lile tusi langu linaishia kabla ya ulimi kucheza.

    Ilinizidi nlivyokuwa nna miaka kama 22 mpaka 30. Ila niliwaficha wazazi wangu ili wasinipeleke kwa sangoma. Ilikuwa nsipochezesha kidole gumba basi tusi laja lenyewe bila breki.

    Cha kushangaza, mi nilikuwa napata A za hesabu na physics mpaka leo.

    Hivyo haihusiani na uwezo wa kimsomo.

    ReplyDelete
  5. Asante mdau kwakunisahihisha nikweli si TROUT SYNDROME KWA USAHIHI NI TOURETTE SYNDROME. Thank younilichanganya kidogo.

    ReplyDelete
  6. Apelekwe kwenye maombi jamani, yupi Nabii Flora hapo Mbezi salasala Dar es salaam, wengi wanapona kwa maombi. Mungu amsaidie na mke wake wote waombewe watapona tu.

    ReplyDelete
  7. Huyu amechanganya mengi... Huu ugonjwa utokana na mawazo ya kupita kiasi tena ya kuhuzunisha. Utakuta mtu anatukana kimoyomoyo kila wakati kwa sabb ya maudhi yasiyo kikomo.

    Dawa yake ni kubadirisha mazingira, na kupata mtu wa kumshauri ( counseling) Afanye mazoezi..

    Mie nilikuwa na rafiki yangu aliyekuwa anakaa na mama wa kambo. Kumbe yule mama alikuwa akimtesa sana, na kumsingizia uwongo kwa baba yake.

    Wakati fulani akaanza kunisimulia jinsi yule mama anavyomtesa, na alikuwa akimaliza sentensi, ni tusi. Ikaendaaaaa. Mwisho wa siku ikawa mazoea.

    Ilichukua kama miaka 2 mpaka watu wakaanza kumzoea hivyo.

    baadaye akawa amechaguliwa kwenda IFM kimasomo. Nikawa nasikitika nikidhani wanafunzi watakuwa akicheka kila mara. Akiwa huo, baada ya wiki mbili tu hiyo hali ilipungua, na ndani ya miezi 2 alikuwa ok. Hii ni kwa sabb alianza kuconcentrate na masomo , ya zamani akawa amesahau.

    Mpaka sasa amemaliza chuo, yuko safi kabisa, amehamia kwake .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...