Adubo Mustafa Omer Enzi ya uhai wake
Picha hapo juu ndiye marehemu Adudo Omer ambaye maiti yake ipo montuary Dallas Texas nchini Marekani tangia Aug 26, 2013 bado wanatafutwa ndugu, jamaa au watu wanaomfahamu marehemu popote pale walipo. Marehemu alizaliwa April 25, 1956.
Marehemu alishawahi kuishi kwenye miji ifuatayo hapa Marekani Lincoln na Omaha miji iliyopo Nebraska. pia alishawahiishi Des Moines naCedar Rapids miji iliyopo Iowa.
Tafadhali tunaomba ndugu au mtu yeyote anayemfahamu marehemu wajitokeze
Tafadhali wasiliana na
Ben Kazora@ 269 873 0937
Viola Mbise @ 405 613 3445
Frank Maji@ 214 674 6666
Ni kabila gani?na kabla ya kukimbilia uko alikuwa anafanya kazi wapi?kwa hapa tanzania kwa kuanzia hapo tutamtafuta nakupata ndugu
ReplyDeleteTatizo ni pale Mtanzania anapokuwa amejiita mkimbizi kutoka Burundi au Sudan; na ukakuta hajawahi kurudi home miaka zaidi ya ishirini. Ikiwa aliondoka kijana akiitwa Robert Mjuni wa Bukoba, na baadaye akabadili uraia na majina kinyemela na kuitwa Adubo Mstafa Omer, ni vigumu kwa ndugu zake kumtambua. Mdau Sweden.
ReplyDeleteTafadhali tuwe wastaarabu watoa maoni hasa kwa jambo la kifo. Tumeshaonyeshwa sura yake. Tusiulize tena ADUBO ni jina la Nigeria au Burundi. Hii yote ni kutafuta maisha. WAHUSIKA WANAOMJUA WAJITOKEZE NA WASEME KAMA HUYU TUNAMJUA NA JINA LAKE HALISI NI RWEGOSHORA AU ROBERT MUJUNI N.K ILI ASITIRIWE VIZURI NDUGU YAO NA ASIZIKWE KAMA MNYAMA.
ReplyDeletePoleni sana kwa msiba.
ReplyDeleteTunamuombea kwa mungu ndugu waweze kupatikana kwa haraka kwani kila mja wake anahaki ya kuzikwa kwa heshma zote.
Roho ya marehemu ipunzike mahali pema peponi. Amen