Katibu mkuu Msaidizi Wizara ya Maji, Bashiru Mrindoko, akitoa ufafanuzi juu ya namna mbalimbali ya Utawala katika sekta ya maji nchini.

Katibu Mkuu Msaidizi, Bashiru Mrindoko akimsikiliza Kiongozi wa msafara wa wataalamu wa maji kutoka nchini Zambia Dk. Ngosa Haward Mpamba waliokuja kujifunza mbinu bora za usimamizi wa rasilimali za maji nchini.
Bi. Sheila Nakazwe kutoka Zambia wakati wa kujitambulisha muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo.
Bw. Simon Kang’omba, kutoka Zambia akijitambulisha kwa wenyeji wake wakati wa utambulisho, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Bashiru Mrindoko pamoja na jopo la wataalamu wa Rasilimali za Maji wa Wizara ya Maji wakiwa kwenye picha ya pamoja na wataalamu wa maji kutoka Zambia waliokuja kujifunza, Ubungo Maji Makao Makuu ya Wizara ya Maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhe.Bashiru Mrindoko,

    Muwakaribishe na ndugu zetu wa Afrika Mashariki yetu kutokea Jamhuri ya Kenya wanaojifanya wanajua kila kitu muwape nao msasa huo kwa faida yao!!!

    ReplyDelete
  2. Afrika kiboko, Wazambia wanakuja Bongo kupata utaalam au ndio Bongo New York?
    Wenyewe wamejitengea pesa ili waje kujirusha Bongo.
    Kweli kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake......

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Pili,

    Pana mazamo Potofu wa kuwa Watendaji wote Tanzania hawafai!

    Hilo sio kweli, pana Maafisa na Watendaji wengi tu ktk Tanzania yetu ambao ni Wachapa Kazi.

    Ndio kama hapo Maafisa wa Zambia wameambua ufanisi Tanzania wamekuja kujifunza.

    Ni vile kwa sasa Utendaji hupimwa , kufuatiliwa na huratibiwa nchi zoe za dunia, ktk Mashirikisho ya Kimaendeleo ya Dunia kama UNDP, UNICEF, UN WORLDBANK , IMF na mengine, hivyo kama nchiikitenda inajulikana na inaonekana.

    Hebu angalia Majeshi yetu ktk MONUSCO huko Congo DRC hao M-23 kimya wamesimamishwa kama sio Wapiganaji!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...