CHINA imeahidi kuleta nchini Tanzania watalii 30,000 katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwakani.
Ahadi hiyo imetolewa leo asubuhi (Jumapili, Oktoba 20, 2013) na Mwenyekiti wa Wakala wa kutoa huduma za usafiri wa China na Hong Kong (China Travel Services - Hong Kong Limited - CTS) Bw. Zhang Xuewu alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jijini Shenzen, China.
Alisema kampuni yake itawandaa mawakala wa usafirishaji watalii ili kuhakikisha kuwa watalii 10,000 wanapatikana kila mwaka ambao kiu yao ni kuja Tanzania. “Wengi wanapenda kutembelea mbuga, lakini hapa nchini wamezoea kuona walio sakafuni, wakija watawaona wanyama live” (akimaanisha kuwa Wachina wamezoea kuona wanyama wa sanamu kwenye makumbusho yao hapa jiji la Shenzen).
Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya tano ya ziara yake ya kikazi ya siku tisa kwa mwaliko wa Serikali ya China alisema haelewi ni kwa nini kampuni hiyo imeweza kupeleka watalii Afrika Kusini na nchi jirani za Afrika Mashariki wakati haina urafiki nazo lakini imeshindwa kuwaleta Tanzania kwenye ambayo ina mahusiano mazuri na ya muda mrefu.
Hivi na china inatalii au wanatafuta kazi.
ReplyDeleteHahahahaha hawa watakua watalii wa kweli au ndio wanasukumiwa huku maana kule maji yamejaa pomoni.
ReplyDeleteChina tunakubali uwekezai wenu,
ReplyDeleteLakini kama mkija Tanzania kwa Visa za Utalii na mfanye hivyo halafu mrejee nyumbani na sio kutumia visa za Utalii mkaja moja kwa moja kujikita nchini na kufanya Biashara !!!
Kuongezeka watalii ni habari njema kwa mapato ya Tanzania, hmahoteli na wadau wengine wanaopata ajira na kuuza bidhaa katika sekta ya utalii. Watalii kutoka China, na nchi zingine wanakaribishwa. Wananchi wenye uwezo pia wapige jeki biashara ya utalii ili tukuze uchumi wetu.
ReplyDelete