Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akitoa utambulisho wa viongozi wakati wa chakula cha jioni kwa ujumbe wa Tanzania na baadhi ya watanzania waishio Marekani.
Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Bank Dkt. Charles Kimei akiongea na ujumbe wa Tanzania na watanzania waishio Marekani juu ya huduma mpya za kibenki kwa ajili ya Diaspora na maboresho ya huduma ya Tanzanite.
Waziri wa Fedha Dkt. Wiliam Mgimwa akiongea machache wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na CRDB ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kulia kwake ni Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula.
Katibu Mkuu Wizara ya fedha Dkt. Silvacius Likwelile aliyesimama akisalimia ujumbe wa Tanzania pamoja na baadhi ya watanzania waishio Marekani kabla ya kuanza kwa hafla ya chakula cha jioni ubalozi wa Tanzania – Marekani.
Kutoka kulia Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Wiliam Mgimwa, Waziri wa Fedha Zanzibar Bw. Yusuph Mzee, Naibu Gavana wa BOT Dkt. Natu Mwamba wakati wa chakula cha pamoja.
Kutoka kulia wachumi Wizara ya Fedha Bw. Pima Patrick na Erasto Kivuyo wakijipatia chakula cha jioni.
Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi Eva Valerian – Washington DC
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...