Na Mary Gwera,
Mahakama ya Tanzania.
JAJI wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.Dr. Stephen Bwana anatarajia kuapishwa kesho (Alhamisi) kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ya nchini Cambodia.
Uapisho huo unafuatia baada ya kuteuliwa kwake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Ban. Ki Moon kwa kushauriana na Mfalme wa Cambodia, Mtukufu Norodom Sihamoni mnamo tarehe. 09.05.2012.
Mhe. Dr. Bwana ataongozwa kiapo na Rais wa Mahakama hiyo aliyeko nchini Cambodia kupitia Video katika Ofisi za WFP zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia 02:45 asubuhi.
Kabla ya uteuzi huo Dr. Bwana ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T) aliwahi kushika nafasi mbalimbali Kama Jaji wa Mahakama Kuu, Seychelles, 1994-1999, Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Seychelles 2004-2009, pia Kaimu Rais wa Mahakama hiyo ya Rufani kuanzia Mwaka 2006-2008.
Mbali na kushika nyadhifa hizo, Dr. Bwana pia aliwahi kuwa, Mshauri wa Benki ya Dunia Kuhusu uboreshaji wa shughuli za Mahakama, Afrika (2003-2008), Msajili, Mahakama ya Rufani (T), 1989-1994, Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania 1989 na Hakimu Mkazi 1974.
Congratulations Dr Justice Bwana, you deserve this position.
ReplyDeleteCongratulation Dr Bwana, we are proud of you as a Nation.
ReplyDeleteHakuna ICC ya nchini Cambodia.
ReplyDeleteMahakama ya Cambodia ni tofauti kabisa na ile ya ICC the Hague. Ankali omba aliyeandika asahihishe