Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kulia) akimvisha
Cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato
Rugainunura ambaye anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la
Darful - Sudan. Hafla ya uvalishaji cheo imefanyika leo Oktoba 30, 2013
katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini
Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( kulia)
akimpongeza Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato
Rugainunura mara baada ya kumvisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Magereza leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza, Jijini Dar es Salaam. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Magereza, Dkt. Kato Rugainunura ni miongoni mwa Maafisa wa Jeshi la
Magereza ambao wanahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful
- Sudan.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini walioshiriki
hafla fupi ya uvishaji cheo kwa Afisa Mwandamizi wa Jeshi la Magereza
ambaye amevishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza na
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani).
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa nasaha
fupi mara baada ya zoezi la uvalishaji cheo kwa Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato Rugainunura( hayupo pichani) ambaye
kwa sasa anahudumu kazi ya Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darful -
Sudan.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Dkt. Kato
Rugainunura(aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali
wa Magereza nchini, John Casmir Minja(hayupo pichani) mara baada ya
zoezi la uvalishaji cheo lililofanyika leo Oktoba 30, 2013 katika Ukumbi
wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam(
Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...