Na.Tamimu Adam - Jeshi la Polisi.
JESHI Polisi Mkoani Mtwara limefanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T.867 aina ya Toyota Carina Saloon likiwa limebeba shehena ya mifuko yenye meno ya Tembo tisini (90) yenye uzito wa kilogramu 222.1 ya thamani zaidi ya shilingi bilioni moja (1,082, 025,000/=)
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara Kamishina Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Steven alisema kuwa gari lilikamatwa
kata ya Maendeleo, wilaya ya Masasi katika barabara kuu ya Tunduru
kuelekea Masasi.
Zelothe alisema kuwa askari wa doria walilitilia shaka gari hilo na kumuamuru dereva kusimama kuonyesha leseni ya udereva ambapo
dereva wa gari hilo hakuwa nayo, ndipo askari alichukua hatua ya
kufanya ukaguzi ambapo alikuta gari hilo limejaza shehena ya mifuko
inayosadikiwa kuwa ni meno ya Tembo.
“Askari
waliamua kulifisha gari hilo kwenye kituo kikuu cha Polisi wilaya ya
Masasi umbali wa kilometa moja kutoka sehemu lilipokamatwa gari hilo,
wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni dereva na mwenzake walikuwa
wakimshawishi askari huyo waelewane ili wampatie shilingi milioni tatu
aweze kuwaachia lakini askari huyo alikataa na kufanikiwa kulifikisha
gari hiyo kituoni” Alisema Zelothe.
Alisema kuwa kabla gari hilo halijasimama vizuri dereva na mwenzake waliruka na kutokomea vichochoroni, juhudi za kuwasaka bado zinaendelea ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
Miongoni
mwa vitu vilivyokutwa ndani ya gari hilo wakati wa upekuzi ni pamoja na
simu moja ya kiganjani aina ya Techno, mizani aina ya tonash, fomu za
“notification” pamoja na Bank slip.
Kutokana
na uchunguzi uliofanyika imebainika kuwa dereva wa gari hilo anatajwa
kuwa ni Oliver Lucas mkazi wa Masasi na mwenzake aliyekuwa naye bado
hajatambulika na inaaminika kuwa tajili wao ni mtu mwenye jina la Hassan
Koko anayejulikana kwa jina maarufu la Twalib Nyoni.
Kamanda Zelothe amewataka wananchi
kuongeza kasi ya kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza
kukomesha biashara hii haramu ya usafirishaji wa nyara za Serikali na kutoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...