Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimpokea
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi cha siku
tatu kinachofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. Katika Hotuba yake
ya ufunguzi, Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane
vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao
cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza na
wajumbe wa baraza hilo kabla ya kufungua kikao cha siku tatu kinaofanyika
katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Mbarak Abdulwakil. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini
Malemi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE)
tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. Wa pili kushoto ni Venance
Ntiyalundura, Katibu wa tawi hilo. Katika kikao hicho Ntunguja aliwaomba
watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta
mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
Sehemu
ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam
Ntunguja (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku
tatu unaofanyika katika Hoteli ya Paradise
jijini Mbeya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (wa tano kutoka kushoto waliokaa),
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa tano
kulia waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (wanne kulia
waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa idara wa wizara hiyo na wajumbe
wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya Kikao cha
siku tatu cha baraza hilo kufunguliwa katika Hoteli ya Paradise, jijini Mbeya
leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...