Wakazi wa eneo la mwenge kwa zaidi ya miaka mitano wamekuwa wakikerwa na kinyesi kinachotokana na kuzibuka kwa chemba za maji taka zaidi ya nane.

Chemba hizo zimekuwa zikizibuka na kutiririsha maji machafu ya kinyesi na kupita katika makazi ya wananchi wa maeneo hayo jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Pamoja na jitihada za viongozi wa mitaa kutoa taarifa kwa wahusika,lakini hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa hadi leo jambo ambalo linatishia kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

Mtandao huu umekusanya matukio mbali mbali katika picha yakionyesha hali ilivyo.
 Hizi ni Chemba mbili ambazo zimesha jaa na Kupasuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hili la Umoja street ambapo sasa panaitwa Kinyesi Street.
 Majani Haya si kwamba yamekuwa Kijani kuna mvua katika kipindi hiki cha Kiangazi lakini ni kwamba Maji machafu yanayo Churuzika kila wakati ndiyo yamesababisha kuwepo kwa hali hii hatarishi
 Unaweza kudhani kwamba kuna watu wanakuja kufanya kazi ya kuzibua hizi Chemba hapa , lakini la hasha zimefunguliwa tuu, hii si chemba ya mtu binafsi lakini ni chemba ya mkondo wa maji Taka.
 Hivi ndivyo inavyo onekana Moja ya Chemba katika mtaa huu.. Chemba hii inakaribia kabisa kujaa na ikisha jaa itasababisha Madhara makubwa sana katika eneo hili, Tayari chemba mbili zimesha fumuka,Kama takataka zinavyo onesha kwamba muda wowote zikiziba basi chema hizi zitaachia na kuanza kumwaga maji hayo machafu. hii imepita ukutani kwa mtu mda wowote inafumuka.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nasty, nasty, nasty! Hivi hakuna Sewer system kama ile ya UDSM Mlimani?

    ReplyDelete
  2. Hivi dawasco wanasemaga wapewe taarifa mara moja na watawajibika! Sasa mbona hawapewi taarifa? Toeni taarifa ili muondokane na kero hiyo.

    ReplyDelete
  3. Wakazi wa Mwenge kwani hatuwajui: ACHENI KUTUPA TAKA KWENYE CHEMBA, UJANJA MWINGI,ONA SASA MNAKULA PARFUM MPAKA.......!

    ReplyDelete
  4. Hali hapo maghorofani mmmmhhh..... naogopa kusema mwezenu3.

    ReplyDelete
  5. Kwa kweli hii hali ni hatari sana,badala ya kulaumu na kuendelea kusubiri serikali(dawasco) wakazi wa eneo hili itabidi wakutane na kujipanga namna ya kukabiliana na hii hali

    ReplyDelete
  6. Jamani mpaka tuwatishie OBAMA ndio msafishe....acheni hizo bwana.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana, mkiona vipi karibuni huku vijijini, hakuna kero kama hizo huku, amani upendo, upepo mwanaaana!!! Maisha ya mjini ndo kama hivyo. Poleni sana, mkipata nauli njooni huku vijijini.

    ReplyDelete
  8. Nakumbuka miaka ya nyuma eneo hilo la Mwenge lilikua la kupigiwa mfano katika mfumo mzuri wa maji taka; lakini sasa ndio hivyo, nini kimetokea?

    ReplyDelete
  9. Mwaka 2007 nilikuwa nimepanga maeneo hayo ambapo mabomba ya maji taka yalibadilishwa na wachina ndipo nilipogundua kuwa WATZ hatuoni mbali kwani yaliwekwa mambomba membamba sana na sishangai kujaa kwa chemba hizo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...