Mwenyekiti wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama ya Jijini Dar, Emanuely Shedo maarufu kama 'MC Fomafoma' akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya tamasha la uzinduzi wa CD na DVD yao ambayo inaenda na kwa jina la 'Namtangaza Kristo' ambayo itafanyika tarehe 13/10/2013 kwenye kanisa lao lililopo Kijitonyama, Dar. Kutoka Kulia kwake ni Mwimbaji Modesti Mogani, Mwimbaji na Mtunzi Oliver Israel.
Kutoka Kulia ni Meneja Mipango wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama,  Onai Joseph, Mwenyekiti wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama, Emanuely Shedo maarufu kama 'MC Fomafoma', Mwimbaji Modesti Mogani, Mwimbaji na Mtunzi Oliver Israel.Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama jijini Dar es Salaam inatarajia kufanya tamasha la uzinduzi wake wa albamu 'Namtangaza Kristo' kwa CD na DVD.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kwaya, Emanuely Shedo alisema nia na madhumuni yao ni kufanya tamsaha la uzinduzi wa kwaya utakaoendana na Jublee.
Aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na live bendi pamoja na kwaya nyingine ambazo zitaungana nao. DVD na CD zitauzwa siku hiyo pamoja na fulana za 'Namtangaza Kristo' ikiwemo pia Key Holder za Kijitonyama. Msikose watu wote hakuna kiingilio (Itakuwa ni bure kabisa).
Wanakwaya wa Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama wakitoa burudani mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ninapenda sana hii kwaya. Wana upako kwa kweli na wanazidi kumeremeta.

    ReplyDelete
  2. Tuwekeeni kiduchu kwenye youtube na sisi wabeba box ughaibuni angalau tuone na kuiagiza moja kwa moja toka DSM.

    ReplyDelete
  3. Halo Ankali.
    Kuna mdau hapo juu ameomba aone japo kiduchu wimbo wa Kwaya kwenye albamu itayozinduliwa Jumapili tarehe 13 Oktoba 2013 .Anaweza kufatilia kwenye link http://www.youtube.com/watch?v=KDRchIZrX1U

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...