Mwenyekiti wa Simba SC, Aden Rage akishangilia na wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya wanaoshabikia Simba baada ya kuibuka washindi katika shindano la kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akitambulisha kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa TBL Mbeya mwishoni mwa wiki.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga, Mohammed Bhinda akimkabidhi Nancy Tibanyenda zawadi baada ya timu yake kushinda mchezo wa kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Wafanyakazi akinamama wa TBL Mbeya wakishindana kuvuta kamba katika hafla ya kuzindua kampeni ya Nani Mtani Jembe kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho mwishoni mwa wiki jijini Mbeya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...