Baada ya kuhudhuria sherehe za ufunguzi, Mhe. Mary Nagu na ujumbe wake walifanya mkutano na Mwenyekiti wa Bodi ya Corporate Council on Africa Bw. Paul Hinks (kushoto kwa Waziri Nagu).
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa U.S.- Africa Business Summit 2013 ukifuatilia sehemu ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyikia Mjini Chicago IL. Ujumbe huo uliongozwa na Mhe. Mary Nagu; Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwekezaji, Juliet Kairuki; Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha uwekezaji Tanzania na Mindi Kasiga; Afisa Ubalozi wa Ubalozi wa Tanzania Washington D.C.
Mhe Nagu akifafanua zaidi baadhi ya maswali yaliyojitokeza baada ya mjadala huo kufungwa wakati wa Mkutano wa Biashara baina ya Marekani na Afrika uliofanyika Chicago Marekani Oktoba 8 - 10, 2013.
Juu na chini ni Mhe. Nagu akijadili umuhimu wa Intellectual Property kutambuliwa na kutambuliwa barani Afrika ili kuhamasisha shughuli za uwekezaji na ukuzaji wa uchumi. Wengine walioshiriki kwenye mdahalo huo pamoja na Mhe. Nagu ni Fernandos Dos Santos; Mkurugenzi Mkuu wa African Regional Intellectual Property Organization na Stephen Mallowah; CEO wa Anti-Counterfeeit Agency ya Kenya.
Ujumbe wa Tanzania kwenye picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Vanu Africa waliomuonyesha Waziri Nagu huduma wanayoitoa kwenye baadhi ya nchi za Kiafrika ili kurahisisha mawasiliano ya simu hususan maeneo ambayo huduma za minara hazitoshelezi. Mhe. Nagu alitembelea mabanda ya maonyesho ya wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali walioshiriki Mkutano huo uliokutanisha biashara baina ya Afrika na Marekani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...