Waziri wa Fedha, Wizara ya Fedha Tanzania Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa katikati akisaini mkataba wa mradi wa umeme wa Rusumo, kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi Burundi Mhe. Tabu Manirakiza, kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika Bw. Colin Bruce
 Naibu Katibu Mkuu, Umoja wa nchi za Afrika Mashariki Dkt. Enock Bukuku akimfafanulia jambo Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula walioko pembeni ni baadhi ya walihudhuria mkutano  wa kusainiwa kwa mkataba wa Rusumo.
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mgimwa akikabidhiwa mkataba na Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika Bw. Colin Bruce mara baada ya kusaini.
Mawaziri wa  Fedha wa nchi tatu, kutoka  kushoto Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Burudi Mhe. Tabu Manirakiza, Waziri wa Fedha wa Tanzania Dkt. Wiliam Mgimwa, Mkurugenzi wa Mkakati na Uendeshaji ukanda wa Afrika Bw. Colin Bruce na Waziri wa Fedha na Mipango wa Rwanda Mhe. Clever Gatete na pamoja na wakitabasamu mara baada ya kusaini mkataba huo
 Ujumbe wan chi tatu Tanzania, Rwanda na Burundi pamoja na Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo.
 Naibu Katibu Mkuu, Umoja wa nchi za Afrika Mashariki Dkt. Enock Bukuku akisoma taarifa
Mkutano ukiendelea. Picha na Bi. Ingiahedi Mduma 
na Bi Eva Valerian – Washington DC: Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Natumai hiyo mikataba mumeisoma vizuri musije kutubebesha zigo kama la Richmond na IPTL hapo baadae.

    ReplyDelete
  2. Ankal,tafadhali picha bila habari si habari: suala hili ni muhimu sana, ebu jitaidi kutupasha haya kuhusu habari hizo:
    je ni nini haswa? Mkataba wa mradi wa umeme wa Hydo/Maji au gesi, diesel, makaa, au upepo (wind) na pia ni Mega watts ngapi? 100MW au zaidi au pungufu, pia ni pesa kiasi gani zimesainiwa US$ ? millions ngapi? Je ni mkopo (loan) au msaada (grant), je mradi utachukua muda gani? napia natumaini umeme huo utakuwa wa kushirikiana Tz, Burundi na Rwanda. asante, alex bura dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...