Mtoto wa muigizaji mkongwe nchini, Mzee Small, Wangamba Mahmud Said Wangamba ameiomba serikali na makampuni aliyoyafanyia kazi baba yake kumsaidia gharama za matibabu ya baba yake yaliyosimama kwa sasa kutokana familia hiyo kushindwa kumudu.

Akizungumza na mtandao wa filamucentral, Mahmud alisema familia imeshindwa kuendeleza matibabu ya Mzee Small kwa muda mrefu kutokana familia hiyo kuwa na kipato kidogo na kushindwa kumudu gharama za matibabu na hivyo kuiomba serikali na makampuni aliyowahi kufanyanayo kazi yaweze kumsaidia.

“Sisi kama familia tunajisikia vibaya sana tunaposhindwa kumsaidia baba kwa sababu yeye ni kila kitu, mimi nasoma sina kipato, mzee toka mwaka jana mwezi wa tano mwaka jana alipomaliza dawa zake hajatumia dawa hadi leo kwa sababu hatuna fedha,”

“Lakini jambo linalotuuma hakuna hata kampuni ambayo imeonyesha kumsaidia kama Bakhresa alikuwa kuwa akifanya nao kazi hakuna msaada lakini pia Serikali kupitia menejimenti utumishi wa umma walikuwa wanafanya nao kazi wamemtosa yupo tu, pengine wanasubiri afe ndio waje kumzika,”anasema Mahmud.

Mzee Small anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi ikiwa sambamba na kupoteza kumbukumbu anahitajka zaidi ya milioni moja na nusu kwa ajili ya matibabu kutokana na ushauri wa daktari kwani inasemekana kichwani kuna tatizo ambalo linamsababishia kupoteza kumbukumbu anahitaji dawa kwa ajili ya tatizo hilo na muda wa kupomzika.

Kwa anayeguswa na tatizo hilo anaweza kuitumia familia yake mchango wa matibabu kwa namba TIGO – PESA 0714 344 039 kumsaidia mzee Small.

Source: Filamu Central

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kwanza kabisa nyie wote mliokua hapo FILAMU CENTRE ni bule kabisa na hamna maana yoyote hapa duniani,bora muanze kufa nyie kulikoni huyo mzee wa watu,nanyie wote wacheza filamu za kitanzania,waongozaji pia ni bule kabisa hamfai pesa mbili,,nasema haya yote nikiwa na hasira kali sn coz siamini ya kwamba nyie wote hapo kwa wingi wenu mkashindwa kumsaidia mwenzenu mpaka anakua katika hali hiyo?,,tuje kwahizo KAMPUNI ALIZO FANYA NAZO KAZI,tuanzie hapo AZAM MEDIA jamani huyo ni MUISLAM mwenzenu mmemzulumu vya kutosha sasa mtubu kwa kuogopa ZAMBI hapa isingekua huyu mtt wake kuweka mambo yote hadharani wengi wetu tusingejua kinachoendelea,,kwa hiyo mchukue hilo jukumu la MATIBABU YAKE MPAKA APONE,hatutaki kusikia anakufa huyu Mzee wetu,,why nakwambieni hivyo? Coz AMEKUINGIZIENI MORE MONEY than mlizokua mnamlipa so huu ndio muda wakuziludisha KWAKE do so plz,,nakwa upande wa SERIKALI wizara inayo husiana na hayo mambo HAKUNA MPANGILIO UNAOELEWEKA wa kuwaweka WASANII wote KWA PAMOJA ndio maana yanatokea mambo kama haya ya AIBU,wasanii kuibiwa kazi zao,kuzulumiwa kwenye malipo yao,kutolipwa vizuri,na kukosekana kwa SHERIA KALI ya kuwaazibu hao wezi wa WASANII,,naitwa mdudu kakakuona nipo huku UINGEREZA,nawapendeni wote huko na mkaee kwa AMANI,

    ReplyDelete
  2. Ni kweli huyu mzee, baadhi ya taasisi za serikali zimemkamua sana,hasa kuhamasisha wananchi katika matamasha mbalimbali.

    Labda wengi watasema si alikuwa analipwa?

    WAJUZI WATAJIBU "ALILIPWA KIINI MACHO"

    Pengine ndio sababu pamoja na kipaji changu chote hali ndio hiyo.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA
    MUNGU BARIKI WALIOMKAMUA HUYU MZEE WAPATE HURUMA.

    MUNGU MBARIKI "MZEE SMALL"

    AMINA.

    ReplyDelete
  3. Yaani million moja tu .Michuzi set up account sir Watu tumsaudie babu Huyu

    ReplyDelete
  4. tusubirie afe tutaenda kuhani na kutoa sifa za marehemu.

    mzee kipara yakikua vivihivi aliteseka san mpaka akaaga dunia

    ReplyDelete
  5. Pole sana mzee small tupo pamoja ktk hili!...Nawakumbusha hasa wasanii wengine anzeni kujiunga BIMA YA AFYA kwa kweli inasaidia sana!

    ReplyDelete
  6. mdau wa mwanzo umesema kweli kabisa lakini mbona hujasema kama utajitolea kumsaidia si bore ya mdau wa tatu kamuomba michuzi a set up account watu wamchangiye usiwe na ghadhabu ya kuropoka ropoka japo kuwa inatia uchungu mdau wa mwanzo fanya action tulete pesa za mama queen tuone mambo okay.

    ahsanteni wote wadau kwa kunganyia mada hii na kuna kweli watanzania popote tulipo we can do it kwa moyo wetu wahuruma

    ReplyDelete
  7. mbunge angekodishiwa ndege akaenda kutibiwa india!!kama msanii hivi, wewe mtu mwenye influence inakuwa vipi? Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote......

    ReplyDelete
  8. Mimi naomba tumtumie mtoto wake kwa njia simu ya mwanawe. TIGO PESA.!!

    ReplyDelete
  9. tumsaidie moja kwa moja huyu Mzee kwa kutafuta Hospital itakayomtibu kwa haraka na kumlipia...Pesa ni shetani isije wengine wakajipatia utajiri kwa matatizo ya mzee wetu alafu hasipone wakati tumeshachanga pesa...Kuanzia watubaki, ndugu mpaka watoto sio wa kuamini pia

    ReplyDelete
  10. Watanzania wote ambao tumeona kazi zake nakufurahia sasa tunatakiwa kuonyesha upendo wetu kwake. Aibu kwao makampuni waliyomtumia kutangaza bidhaa zao kama Azam kushindwa kumsaidia kiasi hicho cha fedha! Mie nimekuwa nikipita hapo Tazara nikiwa kwenye basi/gari naona matangazo ya mzee Small kuhusu bidhaa za Azamu, binafsi naomba ujumbe huu umfikie mzee Bakharesa labda hajui hilo kabla hatuja laumu kuhusu kiwango chake cha Corporate Responsibility.
    Michuzi tufahamishane njia itakayokuwa imeandaliwa kama mdau hapo juu alivyopendeza kufunguliwa a/c tumchangie watanzania wenzake. Kama kuna makampuni yatajitokeza kumfadhili pia tufahamishwe ili nasi wananchi tuone namna yakulipa fadhira ya uteja kwa bidhaa zao kwani inabidi tuanze kuona ni makampuni gani yanajali jamii inayowafanya waendelee kibiashara.

    ReplyDelete
  11. Hakuna aliyefikiria kama accountant hapo,,...ni muhimu kuhakikisha ukweli ya yanayosemwa hapo before kuanza kutigo pesa tu au kusetup account,..hata wewe unaweza kumakeup stori kama hio na ukatumiwa tu pesa,...Mkaguzi King Jojo.

    ReplyDelete
  12. Mdau wa tano unamaanisha nini "tuko pamoja katika hili". Ushaambiwa zinahitajika 1.5mil wewe unaleta maneno matupu yasiyo na maana. Wadau wa 3 na 8 wameongea mambo ya akili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...