Timu ya soka ya Mwananyamala jana iliibuka bingwa wa kombe la Meya wa Kinondoni na kukabidhiwa zawadi za bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi. 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo,Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba aliwaasa vijana hao kutumia vema zawadi hizo ikiwemo fedha na bajaj kwa kusaidia maendeleo yao ikiwemo kuboresha maisha yao. 

Makamba alimsifu Meya wa Manispaa hiyo,Mh Yusuph Mwenda kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yanasaidia kuwaleta vijana pamoja na kudumisha mshikamano na amani baina yao. 

Kwa upande wake Meya wa Manispaa hiyo,Mh Yusuf Mwenda alisema huo ni mwanzo tu wa kampeni yake ya kuweka safi manispaa yake ambapo kupitia michezo anawahamasisha wakazi wa manispaa hiyo kuweka safi mazingira yanayowazunguka.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba (kushoto) akizungumza na wakazi wa Manispaa ya Kionondoni. kushoto kwake ni Meya wa Manispaa hiyo,Mh. Yusuph Mwenda na Naibu Meya wa manispaa hiyo,Mh. Songoro Mnyonge.
Mshambuliaji wa Mwananyamala,Rashidi Kidebe (kushoto0 akiwania mpira na beki wa Kawe Kombaini Emmanuel Nengu, wakati wa mtanange wao wa fainali ya Kombe la Meya wa Kinondoni,katika mchezo uliopigwa jana jioni kwenye uwanja wa Magunia,Msasani jijini Dar.
Naibu Maziri wa Mawasiliano, Mayansi na Teknolojia,Mh. Januari Makamba (kushoto) akikabidhi funguo ya pikipiki ya matairi mawili kwa mwamuzi wa nje wa michuano hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...