PSPF sasa si kwa watumishi wa umma pekee bali hata wanamuziki, waigizaji, wachezaji na hata watu wengine waliokwenye sekta zisizo rasmi wanaweza kujiunga na kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.

Wadau wengi wa tasnia ya sanaa na michezo walijitokeza kwenye halfa hiyo tukianza na Elizabeth Michael Lulu, Mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi, Flaviana Matata, Mtitu, Steve Nyerere, Nahodha wa timu ya taifa ya soka wanawake Sophia Mwasikili na wadau wengine kibao wa tasnia ya filamu Tanzania.

Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata
Steve Nyerere

Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin

Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin anasema lengo kukukutana na wadau hawa ni kutambulisha kwao mpango wa uchangiaji wa hiari (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME-PSS) ambao unamwezesha mtu yeyote kujiunga na mpango huo awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe.

“Uzuri wa mpango huu wa uchangiaji wa hiari, unaruhusu hata wanachama waliokwenye mifuko mingine kujiunga nao lakini pia mwanachama anayohiari ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria yaani Main Scheme” Anasema Costantina

Anasema kuwa kiasi cha michango kwenye mpango wa hiari kinaanzia shilingi elfu kumi (10,000) kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu ambapo mwanachama yuko huru kuchagua kuwasilisha michango kwa wiki, mwezi au kwa msimu na michango hiyo inawasilishwa kupitia akaunti ya benki, au wakala wa malipo wa M-Pesa na Airtel Money.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu anasema mpango wa hiari ni mkombozi kwa wadau wa sanaa na michezo kwa kuwa utawawezesha kujiwekea akiba itakayowasaidia wakati na hata baada ya kustaafu kufanya shughuli zao.

Katika kuhakikisha kuwa elimu ya uhifadhi inawafikia watu wengi na kuwahamasisha kujiunga na mpango huo wa hiari PSPF imekusudia kuwafanya wasanii na wanamichezo kuwa mabalozi katika kufikisha elimu hiyo kwa jamii.


“Sio jambo rahisi kuielimisha jamii juu ya kujiwekea akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye lakini kupitia wasanii na wanamichezo tunaweza kuleta mabadiliko na kufanya watu wengi kuwekeza katika mifuko ya hifadhi ya jamii” anasema Mayingu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Duuuh kweli Steve Nyerere anafanana na Julius Kambarage Nyerere!

    Tazama anavyo andika hapo ni kama JKN alipokuwa kijana akiwa Mwalimu wa Shule.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...