Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Swissport katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere wakati akielekea kwenye ndege jioni ya jana, Jumatatu, Oktoba 28, 2013, kwenda London, Uingereza, kwa ziara ya kikazi ya siku nne ambako atahudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Serikali Uwazi (Open Government) uliotishwa na Serikali ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Mheshimiwa David Cameroun. Kushoto kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe na kulia kwake ni Meneja wa Shirika la ndege la Emirates uwanjani hapo Bw. Aboubakar Jumaa. (PICHA NA IKULU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Inaonekana hapa kama vile mheshimiwa Rais na msafara wake hakutumia ndege yake badala yake emirates halafu yuko kwenye hii terminal ya abiria kawaida. Big up Mr.President kwa kubana matumizi ya serikali.

    ReplyDelete
  2. Nadhani ndege ya Raisi ipo matengenezo.

    Mara zote sisi Tanzania Raisi wetu ni mmoja wa Maraisi wachache ktk Afrika ambao wanatumia Presidential Jet.

    Na pia tusichukulie kitendo cha kutumia Ndege ya Raisi ni anasa, la hii pia ni Heshima ya kuwa nchi yetu si haba angalau tunajiweza!!!

    Tukumbuke ndege ya Raisi ina vitu vitatu vinavyotujengea heshima.

    1.Nembo ya nchi (Adam na Hawa),
    2.Bendera ya nchi mkiani,
    3.Jina la nchi.

    Ndege ya Raisi itengenezwe haraka sana!!!,,,tafadhali.

    ReplyDelete
  3. leo ninaona msafara wamaraisi unapitaa hapa silver town ila uzuri wa ulayaa utapwea escort hakuna mambo ya kusimamisha magari hapaa...kama tz kutiliana hasara za kijinga..

    ReplyDelete
  4. Rais anajitahidi anastahili usafiri ktk mizungunko yake kwa maslahi ya nchi.lakini namshauri akemee RUSHWA .vinginevyo maendeleo ya nchi ni kama kuweka maji kwenye ndoo inayo vuja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...