Kuna UTAPELI mpya umeingia Nchini, kuna watu ambao wanajifanya wana makampuni na wanatafuta watu wa kazi namaanisha wanatangaza nafasi za kazi, nafasi hizo za kazi huzitangaza kupitia mitandao ya Internet ambayo huwa ina maeneo ya kutangaza nafasi za ajira, nitashindwa kuitaja mitandao hiyo kwa kuwa sio utaratibu ila wewe ambaye unajua kuwa kuna mitandao ambayo inatangaza ajira kupitia njia ya Internet ujue ndio hiyo ambayo tunaiongelea hapa. 

Matukio yenyewe yanakuwaje: 



Watu hao hutangaza nafasi za kazi mbali mbali kupitia mitandao hiyo kwa kuandika wana makampuni na wanatafuta watu kwa nafasi mbambali kwenye makampuni yao feki, kwa kutambua watanzania wengi wana shida ya ajira hutangaza nafasi ambazo wanaamini wengi wataziomba na kuweka vigezo vya chini sana hasa eneo la Elimu na uzoefu kwa kuamini wengi wataomba, baada ya hapo, wewe mwenye shida ya ajira ukishatuma CV yako ambayo itakuwa pia inaonyesha mawasiliano yako, wao hutumia mwanya huo kukutumia ujumbe mfupi (SMS) na kujifanya wao ni wafanyakazi wa kampuni husika ambayo imetangaza nafasi hiyo na kujidai  wanaweza kukusaidia kuipata kazi hiyo na kukutaka uwatumie hela ili wakufanyie mpango na kukutumia maswali ambayo utaulizwa kwenye INTERVIEW na majibu yake, hawa jamaa kwa kutambua shida ya Watanzania hawasemi wanataka kiasi kikubwa huwa wanataka kiasi cha Elfu kumi hadi Hamsini, wanafanya hivyo kwa kutambua wewe mtafuta ajira unaweza ukakipata kiasi hicho. 

Matapeli hao hudiriki kukwambia na kiasi cha mshahara ambao utalipwa kwenye kazi hiyo ili kukutamanisha utume hiyo hela, simu hiyo ambayo imekutumia ujumbe huo ukiipigia huwa haipatikani na ikipatikana haipokelewi na wanakua wameziregister kwa majina ambayo wanakuaminisha ni yao kumbe ni majina ya uongo ya kutapelia watu. 

Mpaka sasa wameshawaliza watu wengi sana kwa hiyo wewe mdau kuwa makini sana wakati unaomba ajira kupitia mitandao mbalimbali ya Internet, ukiona unaombwa hela baada ya kuomba ajira kupitia mitandao hiyo ujue ndio hao matapeli. 

KUWA MAKINI EWE MTANZANIA

IMETOLEWA NA: 
MDAU MPENDA HAKI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ahsante kwa taarifa

    ReplyDelete
  2. Lakini na wewe unaetegemea kutoa rushwa ili kupata kazi Fulani, kwa kuazia, wewe mwenyewe ndio chanzo cha matatizo.. na inaelekea hujiamini na pengine huna credential nzuri..Kwa mtu anaejiamini na mwenye cheti kizuri na qualifications zinazotakiwa hawezi ku-fall in that silly trap..

    ReplyDelete
  3. Thobias Odhiambo ChachaOctober 20, 2013

    wandugu tuwe makini na hawa matapeli.

    ReplyDelete
  4. Hii ni Kanyaboya ya Lugha pia!

    ReplyDelete
  5. Asante ndugu. Nikiona tena hayo matangazo kwenye hiyo mitandao nituma CV feki halafu niwakamate. Kusajili simu kwa jina la uongo ni kosa la jinai just for starters!

    ReplyDelete
  6. Asante sana mdau kutuhabarisha. Tutachukua tahadhari.

    ReplyDelete
  7. Siku ya shida ya Nyani mvua hunesha na hata miti hutereza!

    Duhhh, kwa minoti hiyo kama 10 Million hivi inayoonekana hapo mtu utaamini Ajira ipo, kumbe lohhh unapigiwa hesabu ya Nyekundu zako kadhaa hivi!!!

    ReplyDelete
  8. Matapeli hao ni kina biija mpola wanaolaghai wengine. When the deal is too god always think twice, they may be a catch somewhere.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...