Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini (hayupo pichani) wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nadhani kuna haja ya kuelimishwa na pia kufahamishwa jinsi ya kuikamata/kuionyesha hii bendera yetu ya Taifa, maana mara kadhaa imekuwa ikikamatwa ndivyo sivyo. Na hii ni kwa mujibu wa mpangilio mzima wa rangi zake tujuwe ni ipi inatakiwa iwe juu na ipi imalizikie chini. Hao vijana hapo nimejaribu kujiuliza ndio tuseme wanai-match na hizo T-shirt zao au...? Lakini naamini ni kwa kutokufaham tu, wao almuradi wamekamata bendera ya Taifa. Na hizo 'top' zao zingependeza zaidi, endapo zingekwenda sambamba na mpangilio halisi kama ilivyo bendera yetu ya Taifa, KIJANI, MANJANO, NYEUSI na kumalizikia na hiyo BULUU kuliko kinyume nyume.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...