Wachezaji wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya Tanzania wakiwa na medali zao za Fedha mara baada ya kutunukiwa kwa kupata nafasi ya tatu katika mashindano ya Pool Afrika yaliyofanyika jijini Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Safari Pool kutoka Tanzania wakishandilia na mchezaji Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) Afrika uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Wachezaji na mashabiki wa timu ya Taifa ya Safari Pool ya nchini Tanzania wakiwa wamembeba mchezaji,Patrick Nyangusi mara baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) kwa kumfunga Vishen Jagdev wa Afrika Kusini 6-4,katika mchezo uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool kutoka Tanzania, Patrick Nyangusi akicheza dhidi ya mpinzani wake, Vishen Jagdev kutoka Afrika Kusini (hayupo pichani) wakati wa mchezo wa fainali uliofanyika Blantyre Malawi mwishoni mwa wiki.
Nadhani kuna haja ya kuelimishwa na pia kufahamishwa jinsi ya kuikamata/kuionyesha hii bendera yetu ya Taifa, maana mara kadhaa imekuwa ikikamatwa ndivyo sivyo. Na hii ni kwa mujibu wa mpangilio mzima wa rangi zake tujuwe ni ipi inatakiwa iwe juu na ipi imalizikie chini. Hao vijana hapo nimejaribu kujiuliza ndio tuseme wanai-match na hizo T-shirt zao au...? Lakini naamini ni kwa kutokufaham tu, wao almuradi wamekamata bendera ya Taifa. Na hizo 'top' zao zingependeza zaidi, endapo zingekwenda sambamba na mpangilio halisi kama ilivyo bendera yetu ya Taifa, KIJANI, MANJANO, NYEUSI na kumalizikia na hiyo BULUU kuliko kinyume nyume.
ReplyDelete