Naibu waziri wa habari utamaduni na Michezo, Amos Makalla akimkabidhi bendera ya Taifa nahodha wa timu ya Taifa ya Safari Pool, Charles Venance wakati wa kuagwa rasmi wakielekea kwenye mashindano ya mchezo huo ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Malawi Octoba 23-26,2013.Makabidhiano hayo yalifanyika Mkoani Morogoro jana.Kulia ni Makamu mwenyekiti wa chama cha Pool Taifa, Fredy Mushina baadhi ya wachezaji wa timu hiyo.
NAIBU waziri wa habari utamaduni na Michezo Amos Makalla ameikabidhi timu ya taifa ya pool table bendera ya taifa kwaajili ya kwenda uiwakilisha nchi kwenye michuano ya afrika mashariki nchini Malawi,ambapo liwataka kwenda kuitangaza nchi kwa mema.
Makala alikabidhi bendera hiyo jana mjini Morogoro na kuwahimiza wachezaji hao kuhakikisha wanakuwa raia wema ili wengine waweze kuiga kutoka kwao sambamba na kuonyesha umoja na ushirikiano.
Alisema Serikali imeanza kuutambua mchezo huo na kuupa ushirikiano hivyo kuipongeza kampuni ya TBL kupitia bia yake ya safari lager ambao ndiyo wadhamini wakubwa wa mchezo huo.
“ Hongereni TBL kwa kazi nzuri mnayoifanya huu mchezo ulikuwa haufahamiki kabisa na sasa unajulikana na kupendwa ni kazi kubwa ambayo mmeifanya inayostahili kuigwa na makampuni mengine” Alisema Naibu Waziri huyo.
Naye Mwalimu anaeinoa timu hiyo alisema anaishukuru timu hiyo kwa kuwa imekuwa ikionesha nidhamu ya hali ya juu tangu wakiwa kambini, nakwamba timu imejiandaa vya kutosha na wanauhakika wakurudi na ushindi
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama cha mchezo wa pool table Tanzania (TAPA) Fredy Mushi aliiomba serikali iuangalie mchezo huo badala ya kungalia michezo mingine, nakwamba kufanya hivyo kutawawezesha wachezaji kuwa na ari ya kufanya vyema zaidi wakati wamashindano kama haya.
Aidha wachezaji wanaokwenda kushiriki michuano hiyo nchini Malawi ni , Kampten watimu hiyo Vernace Charles, Omary Akida, Festo yohana, Mohamed Idd, Mercxedek Amedius,Godfrey Swai, Abdala Husein, na Patrick Mnyanguzi.
Mashindano hayo ambayo yanataji kuanza kutimua vumbi Oktoba 23 hadi 26 yanatarajia kushirikisha nchi 14 kutoka afrika ambazo ni Kenya , Tanzania,Afrika ya Kusini,Zambia, Lesotho,Kongo, Swazland, Ghana,,Nigeria, Misri, Morocco, Namibia, Msumbiji, na Mwenyeji Malawi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...