Mchakato wa kutafuta Washiriki wa Kambi ya Tanzania Top Model ulioanza miezi miwili iliyopita utakamilika kesho Jumapili katika ukumbi wa Lamada Appartment iliyoko Ilala Dar es salaam.

Audition ya Kesho itakamilisha idadi ya Wasichana 20 watakaochaguliwa kutoka maeneo mbalimbali nchini na watakaounda kambi ya Taifa ambayo itaendeshwa kama Tamthilia halisi kwenye kituo kimojawapo cha Televisheni, Usaili wa kesho, utakuwa ni mgumu sana kwa sababu tunategemea wasichana wengi watajitokeza wakati nafasi zilizobakia ziko kidogo.

Watakaochaguliwa kesho, wataungana na wenzao Zulfar Bundalah, Darline Mmari, Nuru Mfaume, Lorrain Clement, Elizabeth Boniface na Irene Kasanda kuwakilisha jiji la Dar es salaam katika mashindano ya Tanzania Top Model yanayotazamiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka.

Baada ya Audition za kesho, Kamati ya maandalizi itatoa wasifu wa kila mshiriki na kutangaza tarehe ya kuanza kwa kambi ya Taifa. Mashindano ya Tanzania Top Model yatakuwa yanafanyika kwa mara ya kwanza nchini na mshindi wake atawakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Top Model of the World yaliyopangwa kufanyika nchini Ujerumani au Misri mapema mwakani.

Hili ni shindano litakalo washindanisha Mabinti wenye ndoto ya kuwa Wanamitindo wa Kitaifa na Kimataifa, na tunaamini kuwa litawajenga na kuwafanya wajiamini zaidi na kuwapatia fursa ya kushiriki kwenye mashindano na maonyesho ya mavazi mbali mbali ya Kimataifa.

Shindano la Tanzania Top Model limeanzishwa ili liwe chimbuko la nyota nyingine katika dunia ya Wanamitindo na kuziba ombwe lililoko la kuwatafuta, kuwatayarisha na kuwatafutia mikataba wanamitindo wa kitanzania ambao ndoto zao zimekuwa ni kubwa katika tasnia hii. Mchakato wa shindano hili umejiegemeza kwenye kuwajenga na na kuwafanya wajiamini na waaminiwe kwa kazi mbalimbali.

Pia kwa kufanya hivi, tutakuwa tumeleta kichocheo kingine cha kuitangaza nchi yetu katika mavazi na sanaa nyingine kimataifa . Hivyo tumeona kuanzisha Shindano hili ili liwe kichocheo kingine cha kuitangaza nchi yetu katika mavazi na sanaa nyingine kimataifa na kuwa chimbuko la nyota nyingine katika dunia ya Wanamitindo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...