Kijana akikaguliwa kwa umakini baada ya kutiliwa mashaka na walinzi wa Mlimani City leo mchana
 
 Mlinzi wa kike akiwasubilia wananwake watakaotaka kuingia kwenye jengo la mlimani city ili hawakague
Ukaguzi ukiendela


PICHA NA PAMOJAPURE/PAMOJA BLOG


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ni vizuri kuchukua tahadhari japo ni kazi ngumu kwakua baadhi ya watu wanaweka ugumu huo mfano huyo dereva Mzalendo anayeweka mbele maslahi ya tumbo kuliko usalama wa binadamu na kudiriki kuwapakia kwa kificho wahamiaji haramu,ingekua vizuri kama hukumu ya watu kama hawa inatangazwa ili wenye uchu wa pesa kama yeye wajifunze.

    ReplyDelete
  2. Hiyo sasa aibu...Hao walinzi pamoja na utaratibu huo wote ni"chai" tupu.Mtu mwenye dhamira mbaya bado anaweza kuwa na sila ya moto,akakaguliwa na isionekane na akaruhusiwa kuingia ndani,..hapo sijui mtaanza utaratibu wa kuweka chumba na kuwavua wote nguo zote ili kubaini hao??!!..Hebu Tanzania tubadilike jamani,hayo mambo ya "cheap labor" ni ya karne ya 18. Nashauri sehemu muhimu na zile za mikusanyiko kama hizi ziwekwe vifaa kama kamera za ulinzi,viakisi(scanners),pamoja na 3D metal detectors ..Hapa hata mtu kama anaweza akimeza kisu kitaonekana tu.TWENDE NA WAKATI..huu unafuu unatutia aibu,mtu ana rungu tu halafu analinda mali ya mabilioni ya fedha,unadhani watakaokuja hapo watakuja na mawe??!

    ReplyDelete
  3. Yan hilo zoezi ni kama igizo na halina tija. Jana jioni nimeenda mlimani city na gari nikasimamishwa akasema wanataka kukagua, akakagua kwa kuangalia kwa macho hana detector yoyote...wkt nakaguliwa magari mengine yakaruhusiwa bila kukaguliwa. Nilipowauliza wanasema eti yakikaguliwa yote wataweka foleni. Nikajiuliza kuna maana gani sasa ya kukagua mmoja na mwingine asikaguliwe. Nilipofika kwy lango la kukaguliwa wkt tunakaguliwa kuna kenta ikawa inashusha mabox ya Tv...yakaingizwa bila ukaguzi wowote. Nikajiuliza kama mizigo inayoingia kwy yale maduka haikaguliwi kuna haja ya kutukagua sisi?

    Naomba uongozi wa mlimani city utambue kuwa ugaidi ni organised crime...with network, financial capability na wanambinu nyingi na za kisasa. Hawawezi kuweka mitutu kwy pochi.

    Hivi wanajua wale wapangaji kwy zile appartments kule nyuma ni kina nani na kazi zao ni nn?

    Naliona zoezi hilo ni IGIZO LISILO NA TIJA

    ReplyDelete
  4. Na assume hao walinzi wana silaha zao (bunduki). Ukaguzi wa aina huu ulikuwa hata pale Westgate. Ila askari wao hawakuwa na bunduki. Inabidi wawe alert kila wakati na mtu anayeleta mashaka awekwe pembeni haraka iwezekanavyo.

    ReplyDelete
  5. Mh...usalama muhimu ila hii itafanya watu wafikirie mara mbili kama ni lazima kwenda kufanya manunuzi kwenye supermarket kubwa

    ReplyDelete
  6. Inabidi wajizatiti zaidi kwani naona wanafanya masihara, jana mimi nilikuwa na siraha ya moto kiunoni na wakanikagua cha ajabu hawakuiona wala ku detect sasa hapo naona umakini haupo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...