Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akihutubia vijana mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) aliyoizindua leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya vijana walioshiriki uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) wakifuatilia kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Mhe. Benjamini William Mkapa (hayupo pichani) leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
 Mmoja wa wadau toka timu ya Let us read Tanzania akimpa maelezo juu ya vitabu mbalimbali viliyotungwa na waandishi mashuhuri ndani na nje ya nchi.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akiwasomea hadithi mbalimbali na kuwauliza maswali mbalimbali watoto ambao ni wanafunzi toka shule mmbalimbali leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

====== ========  =======
RAIS MSTAAFU MHE. BENJAMINI WILLIAM MKAPA AZINDUA KAMPENI YA TUSOME TANZANIA (LET US READ TANZANIA CAMPAIGN).
Na Benedict Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam.
11/10/2013.
RAIS Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa amezindua rasmi Kampeni ya “Tusome Tanzania (Let’s read Tanzania Campaign) iliyoandaliwa na wadau mbalimbali nchini wenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali.

Katika uzinduzi huo, Mhe. Mkapa ameipongeza kamati ya wadau waandaaji wa kampeni hiyo kwa kujitoa kwao katika kuhakikisha kuwa watoto wa shule ambao ndiyo taifa la kesho wanapata kujionea wenyewe na anatumaini kuwa watahamasika kupenda kujisomea kwa manufaa ya maisha yao.

“Tabia ya kusoma inamjenga mtu kifikra na kumpa mtu mtazamo”. Alisema Mhe. Mkapa. Mhe. Mkapa ameongeza kuwa kwa kuwa elimu haina mwisho, kusoma ni namna ya kujielimisha siku hadi siku na kufungua mambo mapya yanayoipa akili changamoto, hivyo amewasisitizia vijana wajijengee utamaduni wa kusoma hasa vitabu vya kiswahili na Kiingereza.

“Someni kazi za Shaabani Robert mwandishi mkongwe wa Tanzania,  someni kazi za Mariam Abdallah, Ngugi wa Thio’ngo , Chinua Achebe, Ole Soyinka na .” Alisema Mhe. Mkapa.

Aidha, Mhe. Mkapa ametoarai kwa wadau waandalizi wa kampeni ya “Let’s read Tanzania Campaign”  kuwa zoezi hilo lisiishie hapo bali liwe endelevu na kuwafikia watu wengi na haswa vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao wa vitabu uhakikishe vitabu hivi vinafika hadi kwenye shule za vijijini na amehamisisha juu ya ujenzi wa Maktaba na kusaidia kuboresha watoto wetu.

Let’s read Tanzania Campaign ni kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi mbalimbali lenye lengo la kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za vijana na kuwasaidia katika maisha yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii safi sn kwa watanzania woote,tusomeni kwa bidii zote watoto kwa wakubwa,napia tujifunze kusoma kwa makundi au mmoja mmoja au wawili wawilin,wito pia kwenu wanafunzi woote mkitoka mashuleni mkasome tena MAKTABA au za hapohapo mashuleni mzitumie vizuri hizo MAKTABA,

    ReplyDelete
  2. Asante Mhe. Rais mstaafu kwa kutukumbusha kusoma vitabu, ninafahamu wewe ni mpenzi wa vitabu na msomaji mkubwa hodari sana wa vitabu, waliokualika kwenye uzinduzi huu wamepatia haswaaaaa safi sana . watanzania tujenge utamaduni wa kujisomea hasa kwa vijana wetu ambao ndio muhimili wa taifa hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...