Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Rhys Torrington akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari waliopata fursa ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo juu ya uanzishwaji wa Televisheni yao ya Azam TV yenye muonekano wa kisasa zaidi na yenye lengo la kukuza michezo mbali mbali hapa nchini,zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Rhys Torrington akionyesha King'amuzi cha Azam TV kwa baadhi ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) waliopata fursa ya kufanya ziara ya kutembelea Ofisi za Kampuni hiyo,zilizopo eneo la Tazara jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi wa Wakuu wa Idara mbali mbali za Kampuni ya Azam Media wakimsikiliza Mkurugenzi wao.
Wazee wa Kazi ndani ya OB Van la Azam Tv,toka kulia ni Meneja Uzalishaji na Ufundi wa Kampuni ya Azam Media,Mehboob Aladdad,Meneja wa Azam FM na Matukio ya Moja kwa Moja,Yahya Mohamed pamoja na Fundi Mitambo wa OB Van hiyo,Saleh Mansoor (alieketi) wakifatilia moja ya kazi zao.
OB Van ya Azam TV ikiwa imetukia tayari kwa lolote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa


  1. nimekua niki jiuliza ni lini TZ media industry itabadilika ia sasa naona mwenye nazo kaamua yaani Hongera sana ila sidhani kama kulikua na point ya kuanzisha digital receiver ungetumia zilizopo baasi

    ReplyDelete
  2. AZZAM FC hiyoooo inapaa!!!

    Huku Klabu Kongwe zikiendelea na Mipango yao ya Kamati za ufundi (RUSHWA NA USHIRIKINA), Klabu changa kabisa inafanya vitu vikubwa saaana.

    Sasa ni wakati wa kuzihama Klabu za 'Kimsukule' za YANGA na SIMBA.

    ReplyDelete
  3. Azam imefunika vibaya sana.

    Yanga S.C-1936.
    Simba S.C-1938.
    Azam F.C -2004.

    Licha ya Klabu za miaka nenda miaka rudi zikiwa na Umri zaidi ya Uhuru wa Tanzania wa miaka 52.

    Miaka ya Yanga na Simba kutesa sasa inahesabika!

    ReplyDelete
  4. Azam Kilabu mpya kabisa na sasa inamiliki Kituo cha Televisheni.

    Kiama ni Yanga na Simba ambazo hata 'Redio mbao' hazija jaaliwa kumiliki !

    Hapa ndio pale mtu anadai ya kuwa yeye haja jaaliwa kuwa na Akiba wakati hata ukiwa na Kipato cha Shilingi 1/= ni wajibu kutumia sehemu na pia kuwa na akiba kwa ajili ya baadaye.

    Kama hukuwa na akiba na Mipango ya baadaye nani atakuwekea akiba na kukupangia ya baadaye?

    ReplyDelete
  5. Mimi kuanzia leo nahamia AZAM F.C!

    Tunaahidi kuwa Kimichezo zaidi na si kiunazi.

    Kamwe Azam isiwe Tawi la Simba ama Yanga.

    Tena tafadhali tusilete U-Yanga na U-Simba ndani ya Azam hii MPYA NA YA MATAWI YA JUU, tunaahidi ni bora tufungwe na Timu ya POLISI-KILWA kuliko kufungwa na Yanga ama Simba!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...