Mshitakiwa, Sharif Mohamed Athuman (31), ambaye ni mshitakiwa namba
moja katika kesi ya Mauaji ya Bilionea wa Madini ya Tanzanite, Erasto
Msuya mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha,
akitoka nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Moshi, muda mfupi baada ya
kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
Mshitakiwa namba mbili, Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38),
anayetuhumiwa na wengine saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa
kumpiga risasi akitoka kwa taabu nje ya mahakama ya Hakimu mkazi
Moshi, baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka huu.
Mmoja wa Washtakiwa katika kesi ya Mauaji, anayetuhumiwa kushirikiana
na wenzake saba, kumuua Mfanyabiashara Erasto Msuya kwa kumpiga risasi
akisindikizwa na Maaskari kutoka katika mahakama ya Hakimu mkazi
Moshi, muda mfupi baada ya kesi hiyo jana kuahirishwa hadi Desemba 11,
mwaka huu.
Washitakiwa Joseph Damian "Chusa" na mwenzake Shaibu Jumanne Saidi
"Mredi", wakimsaidia Mshitakiwa mwenzao kupanda katika Gari la Polisi
muda mfupi baada ya kesi inayowakabili ya mauaji ya Bilionea wa Madini
ya Tanzanite, Erasto Msuya kuahirishwa hadi Desemba 11, mwaka
huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...