Washiriki wa mkutano wa 7 wa Mapitio ya Utendaji
wa sekta ya Uchukuzi, wakijitambulisha kabla ya mkutano huo wa siku mbili
kuanza katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Jubilee. Mkutano huo wa 7 unawakutanisha wadau mbalimbali wa sekta
ya Uchukuzi kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta na kuzitafutia
ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban
Mwinjaka akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Mkutano 7 wa mapitio ya utendaji
wa Sekta ya Uchukuzi(JTSR 2013), unaofanyika katika ukumbi wa mikutano Jengo la
Golden Jubilee tarehe 28-29 Oktoba 2013. Mkutano huo wa 7 unawakutanisha wadau
mbambali wa sekta ya uchukuzi kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili
sekta ya uchukuzi na kuzitafutia ufumbuzi ili kuboresha Uchukuzi nchini
Tanzania.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Alhaj
Mussa Iyombe, akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 7 wa mapitio
ya utendaji wa Sekta ya Uchukuzi leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano katika Jengo
la Golden Jubilee.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison
Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 7 wa mapitio ya
utendaji wa sekta ya Uchukuzi leo asubuhi katika ukumbi wa mikutano uliopo
kwenye Jengo la Golden Jubilee(PSPF BUILIDNG). Mkutano huo wa siku mbili unakutanisha
wadau wa taasisi mbalimbali za sekta ya uchukuzi kujadili njia mbalimbali za
kuboresha sekta ya Uchukuzi.
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe (wa
tatu kutoka kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi, wahisani
wa Miradi ya Maendeleo na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano wa 7 wa mapitio
ya utendaji wa sekta ya Uchukuzi, Unaofanyika tarehe 28-29 Oktoba katika ukumbi
wa mikutano wa Jengo la Golden Jubilee. Wa kwanza kushoto waliokaa ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mrs. Monica Mwamunyange, kulia kwa Waziri
Mwakyembe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu
ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya Uchukuzi , Bw. Aunyisa
Meena, akiwasilisha mada kwenye mkutano wa 7 wa mapitio ya utendaji wa sekta ya
Uchukuzi, unaofanyika Tarehe 28-29 Oktoba katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la
Golden Jubilee. Mkutano huo utajadili maswala mbalimbali yanayohusu sekta ya
Uchukuzi.
Habari na picha na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini-Uchukuzi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...