Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (kulia) akipokea mfano wa tiketi ya ndege kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana (kushoto), ambayo itatolewa kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. PW pia ni msafirishaji mkuu wa mbio za Rock City Marathon 2013. Wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza, na Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi. Grace Sanga
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kulia ni Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta aliyetangaza zawadi zilizoboreshwa kwa mshindi wa mwaka huu, na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (Kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi za mbio za Rock City Marathon mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana ambaye alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana
Mratibu wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (wapili kulia) akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza zawadi za mbio hizo kwa mwaka huu. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana ambaye alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza na kulia ni Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International Ltd, Bi. Grace Sanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...