ZAIDI ya Wanawake 8,700 hufariki duni kila mwaka nchini Tanzania kutokana na matatizo ya ujauzito na hasa wakati wa kujifungua. Takwimu hizi zinaonesha takribani wanawake 24 hupoteza maisha kila siku huku ikikadiriwa mmoja kufa kila baada ya saa moja.
Hata hivyo wataalamu wa afya wanasema moja kati ya sababu zinazochangia vifo hivi  ni kukosekana kwa huduma za dharura katika Vituo vya Afya wakati wa kujifungua. Hata hivyo Serikali ya Tanzania mwaka uliopita katika ahadi zake imeahidi kupunguza vifo hivi kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015.
“Si sahihi mama mjamzito kufa wakati wa kujifungua au si sahihi mama huyu kupoteza uhai wake kwa kuugawa kwa kiumbe anachokileta duniani, hii haiwezi kukubalika. Na inasikitisha zaidi pale maisha ya mama huyu yanapotea hata kwa mambo ambayo yanaweza kuzuilika,” anasema Rais Kikwete katika hotuba yake mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (U.N) Ban Ki-moon.
Wewe pia unaweza kushiriki katika kupigania kutokomeza vifo hivi kwa akina mama wajawazito pamoja na watoto. Je, unataka kushiriki? Tafadhali fuata kielelezo/link hii hapa chini:-

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...