Taasisi inayosimima uhifadhi na matengenezo ya nyumba za Serikali imeshauriwa kuifanyia marekebisho yaliyosalia Ikulu ndogo ya Kibweni ili itumike vyema katika maadhimisho ya Sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964. 
Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofanya ziara fupi ya kuikagua nyumba hiyo iliyopo pembezoni mwa Makao Makuu ya Kikosi cha kuzuia Magendo Zanzibar { KMKM } Kibweni Wilaya ya Magharibi Mkoa wa Mjini Magharibi. 
Balozi Seif ambaye ameridhika kiasi na hali halisi ya mazingira ya Ikulu hiyo alisema ni vyema nyumba hiyo ya Serikali ikapangiwa taratibu za kutumika badala ya kuachwa ikikaa bure . Alisema Serikali katika kipindi kirefu imekuwa ikipokea wageni wa Kitaifa na Kimataifa wenye hadhi ya kuishi kwenye nyumba hiyo lakini wengi kati yao wanaishia kuwekwa katika Hoteli za Kitalii jambo ambalo linaweza kuepukwa. 
Aliwataka wahusika wa matengenezo ya nyumba za Serikali kuhakikisha kwamba nyumba hiyo { Ikulu } inakamilishwa hitilafu ndogo ndogo zilizobakia ili iweze kuhudumia wageni watakaoalikwa kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za Mapinduzi kutimia Nusu Karne. 
“ Tunatarajia kupokea wageni wengi wa Kitaifa na Kimataifa katika sherehe zetu za mwaka ujao . Hivyo kwa hadhi ya nyumba hii tunaweza baadhi yao kuwapangia wakampumzika kwa kutwa moja kabla na baada ya sherehe zetu kabla hawajarejea nyumbani “. Alisisitiza Balozi Seif. Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza wasimamizi wa Ikulu hiyo ya Kibweni kwa hatua wanazozichukuwa katika kuihudumia nyumba hiyo kongwe. 
Alisema mazingira bora yaliyopo hivi sasa kwenye nyumba hiyo yanaruhusu kwa baadhi ya Mikutano na Kazi za Viongozi Wakuu wa Serikali kuzifanyiwa katika eneo hilo. 
Mapema Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Nd. Salum Maulid alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba tatizo liliopo hivi sasa katika nyumba hiyo ni marekebisho ya jiko la kupikia pamoja na huduma ya maji ambayo haipatikani kikawaida. 
Nd. Salum alisema huduma hiyo ya maji safi hupatikana kwa nadra katika kipindi kirefu tatizo ambalo linahitaji kufanyiwa utafiti wa kina na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.
  Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Nd. Salum Maulid akimtembeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika baadhi ya sehemu za nyumba ya Ikulu ndogo iliyopo Kibweni Wilaya ya Magharibi.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwaagiza wahudumu wa Ikulu ndogo ya Kibweni kuhakikisha kwamba mazingira ya nyumba hiyo yanaendelea kuwa mazuri.
Jengo la Ikulu ndogo iliyopo Kiwebi Wilaya ya Magharibi ambalo linatarajiwa kuhudumia baadhi ya wageni watakaoalikwa hudushuria sherehe za Maadhimisho ya Kutimia Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jengo linahitaji rangi, hata km ni a zamani, kuna rangi zisizopauka haraka siku hizi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...