Muwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Balozi Samantha Power jana Jumatano ( Nov27) alifika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, na Kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Muwakilishi wa Kudumu, Balozi Tuvako Manongi. 
 Balozi Power alitumia fursa hiyo kujitambulisha kwa Balozi mwenzake kufuatia kuteuliwa wake hivi karibuni na Rais Barack Obama kuwa muwakilishi wake katika Umoja wa Mataifa. Katika mazungumzo yao yaliyochukua takribani nusu saa, Mabalozi hao wawili, walijadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa na kitaifa yakiwamo ya uhusiano na ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Marekani na vilevile walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu vipaumbele vya nchi zao katika Umoja wa Mataifa na namna ya kukuza na kuendeleza uhusiano na ushirikiano huo.
Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,  akimkaribisha mgeni wake,  Balozi Samantha Power ambaye ni Muwakilishi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Power alifika katika ofisi za Uwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwa lengo la kujitambulisha na kuzungumza na mwenyeji wake
Karibu sana Tanzania  ndiyo anavyoelekea kusema Balozi Tuvako  Manongi kwa mgeni wake Balozi Samantha Power.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Huyu Bi Nguvu anaoenakana mbabe na mcheshi kweli kweli.

    ReplyDelete
  2. Ucheshi hasa. Naona wameshibana hawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...