Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kimewaandikia barua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe na Mjumbe wa kamati Kuu Dk Kitila Mkumbo ambazo wanapaswa kujieleza kwa siku kumi na moja, kisha watapata fursa kujieleza mbele ya kamati kuu maalumu kwa nini wasifukuzwe kutoka Chamani. 
 Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa habari na Uenezi John Mnyika alisema barua hizo zipo tayari na wahusika watapatiwa wakati wowote kuanzia leo. Mnyika alikuwa akitoa taarifa ya kikao cha Utekelezaji cha sekretarieti ya chama hicho iliyoketi baada ya mkutano wa kamati kuu iliyoketi tarehe 20 – 22 Novemba mwaka huu. Ni katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu alisema kuwa mkutano uliofanywa na Zitto na Dk Kitila mbele ya waandishi hawajazungumzia tuhuma zinazowakabili, badala yake walichofanya ni kujitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizo wavua nafasi zao. 
 Lissu alisema, Zitto na Dk Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa masuala ya PAC, Uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye operesheni za chama au sababu zingine, na walitaja hizo sababu ili kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii: 
“Walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" (kubadili mwelekeo) wa mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya Chama. anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu" alisema Lissu. 
 Aliongeza kuwa CHADEMA kina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na kamati kuu, Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwanini wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika kamati kuuu Aidha Lissu alieleza kuwa Dk Kitilla anapotosha umma na wanachaka kwa kauli yake kuwa kamati kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya ujumbe wa kamati kuu maana amechaguliwa na baraza kuu, alimtaka Kitila na Zitto waangalie vema katiba ya chama hasa majukumu ya kamati kuu, pale yanaporuhusu Mwanachama yeyote kusimamishwa au kufutiwa uachama harka kama kamati kuu itaona kuna umuhimu wa kufanya vile. 
 Kigaila alisema, Kamati kuu iliyoketi Novemba 20-22/2013 ilipitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama ifuatavyo:- 22/11/2013-14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa wanachama, 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji, 16 januari 30 Januari 2014 Rufaa naukaguzi, ambapo tarehe 01 Februari hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi. CHADEMA pia ilisema 16 Februari hadi 29 mwezi huo huo ni kusikiliza rufaa na ukaguzi, ambapo uchaguzi wa majimbo utaanza rasmi 1 Aprili hadi Aprili 10, huku uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi mei 5 mwaka 2014, na ngazi ya Mikoa ni 20 Mei hadi 25 Mei. 
 Huku uchaguzi wa kanda ukitarajiwa kufanyika Julai 9, na haada ya hapo Julai 23 hadi Julai 30 utakuwa ndio muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha uchaguzi wa ndaniya chama. Source: 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Waongo Chadema,mnavita vya ndani kugembea uflame na umangi meza,na
    mlipofikia watanzania tunajua wazi sasa hizi mtafunga tulubai mlale matanga ya marehemu CHADEMA,
    Mbona hizo karatasi ni feki amzionyeshi hadharani ? mnawaogopa akina Zitto wenzenu wanaijua siasa

    ReplyDelete
  2. I don't like this show of stratergy meeting. Haikisaidi chama.

    ReplyDelete
  3. Mnyika alitamka kuwa Mtetezi wa "wahaini" alitamka Katiba kumbe ni Kanuni za Chama. Je, Kanuni za Chama si sehemu ya Katiba ya Chama?

    ReplyDelete
  4. zitto kashikwa!!!

    ReplyDelete
  5. watz hapa sio zitto wala mbowe chanzo cha mgororo huu ni mbowe kubadili katiba pasipo baraza kuu na kamati kuusika katika suala la ukomo wa kugombea nafsi za juu ambapo ilikuwa ni ukomo wa awamu mbili tu na si vinginenyo ndiyo chanzo na mgogoro huu mbona lisu anazunguka mbuyu na mnyika wake chanzo ni hicho jaman kuwa wakweli ili kuokoa chama kutoa wenye akila akabali akina lema na peter msigwa ambao hawajengi hoja zozote bungeni.

    ReplyDelete
  6. Mambo ya chama waachie wenyewe Chadema, usije ukatoa maoni kumshutumu mtu au chama kwa kutojua yaliyomo ndani. Kimsingizi tunataka vyama vinavyoweka taifa mbele na kuchukizwa na ufukara wa nchi yetu na watu wake. Tatizo letu watanzania tunapenda ushabiki badala ya wajibu. Hii haitatusaidia sana karne hii ya 21.

    ReplyDelete
  7. hizo details walizitoa wapi?? na kama walizitoa kwenye laptops za wahusika je sheria za nchi zinasemaje kuhusu ili swala la mtu kuchukua taarifa za mtu binafsi bila ya ruhusa yake?? (privacy and confidentiality of an individual information)

    ReplyDelete
  8. JAMANI JAMANI CHADEMA NILIKIPENDA LAKINI KWA MWELEKEO HUU........ MASIKINI ZITO.

    HAKI YA NANI MKIMTOA ZITO CHADEMA KITAKUFA RASMI OHOOOOO!

    ReplyDelete
  9. CHADEMA MKIWAFUKUZA ZITTO NA DR MKUMBO AU MKISABABISHA WAJITOE MSAHAU KUSHIKA DOLA 2015 NA HATA 2020!

    HIZO SIO NJAMA WALA USALITI NI STRATEGY. LAZIMA MJUE KUWA MPANGO WAO BAADA YA KUKAMILIKA WANGEUWEKA MBELE YA CHAMA ILIKUOMBA KURA NDANI YA CHAMA. KURA ZA WENGI ZINGEKUBALI PENDEKEZO LAO AU KULIKATA KIDEMOKRASIA. INAWEZEKANA PIA KUNGEKUWA NA MAPENDEKEZO MENGINE. SASA MLITAKA WASIFIKIRIE MBELE WAKAE TU KAMA MBUMBUMBU?

    KAMA PENDEKEZO LAO, KWA MFANO LINGEKUBALIWA AU KUKATALIWA, KIKUBWA NI USHINDI WA CHAMA KUCHUKUA DOLA. NDIO MAANA WATU WANNE TU WALIFIKIRIA, WAKASTRATEGIZE, WAKAMUONA OBAMA ANAFAA, WAKAPANGA MIKAKATI WAKAENDA KUMUONA KUMUOMBA. ALIKUBALI BAADA YA MUDA MREFU SANA KUFIKIRIA. LEO USHINDI SI WA HAO WANNE, WALA WA OBAMA PEKE YAO, USHINDI NI WA DEMOCRATS.

    JIFUNZENI. YAMALIZENI NDANI VINGINEVYO MMEKWISHA.

    ReplyDelete
  10. Chadema hiyoo inaelekea KABURINI !!!

    ReplyDelete
  11. Dhambi ya Ubaguzi inawamaliza CDM!

    Tujiandae na Misururu na Mafuriko ya Wanasiasa wa Upinzani na hasa hawa Wachagga kuelekea Chama Tawala.

    ReplyDelete
  12. Haka ni kamchezo. Hatujawakabidhi nchi mnakulsna namna hii, Je! Tukiwakabidhi madaraka itakuwaje

    ReplyDelete
  13. Hata chaguzi hazijaanza kumeshaanza vita vya wenyewe kwa wenyewe je wakipewa nchi itakuaje????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...