Na  Francis Godwin Blog 

FUNDI  magari  mkazi  wa kijiweni  katika  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Bw Abdul Husein (31)  amejikuta  akitupwa  jela  mwaka  mmoja na faini  ya shilingi 200,000 baada  kutiwa  hatiani  na mahakama  ya mwanzo bomani  kwa  kosa la kutaka  penzi  la nguvu  kwa  mwanafunzi  wa darasa la tano  .

Fundi  huyo ambaye  anadaiwa  kukaribishwa katika  nyumba  hiyo   kama mlinzi wa  watoto  wawili  akiwemo mwanafunzi  huyo wa miaka 11 alitenda  kosa  hilotarehe 4 mwezi huu  majira ya saa  3 usiku  baada  ya  kurejea kutoka katika shughuli  zake.

Akisoma   hukumu  hiyo  leo  hakimu  mkazi  wa mahakama  ya mwanzo bomani  mheshimiwa Alois Masua   alisema  kuwa  katika   ushahidi  ambao  ulitolewa mahakamani  hapo na mtoto  wa kiume wa miaka 9  ulidai  kuwa kijana  huyo siku ya  tukio baada ya  kufika  nyumbani alimtaka  binti  huyo  kumpa  sahani  ili  aweke  chips ambazo  alikuja  nazo .

Kuwa baada ya  binti huyo jina  limehifadhiwa na mtandao  huu kumpa  sahani  ndani ya dakika  chache  aliomba  kupewa maji  na binti  huyo alifanya  hivyo baada ya kupewa maji kijana  huyo alimtaka  binti huyo  kusogea  kukaa  katika  eneo kochi ambalo  fundi  huyo amekuwa akilitumia kama  kitanda  chake   sebuleni kama mlizi bado  binti  huyo aligoma  kuingia majaribuni .

Hata  hivyo  haikuishia hapo  baada ya  muda  fundi  huyo fataki  alimtaka  binti  huyo kumsindikiza chooni bado  binti  alionyesha msimamo  wa kutamani masomo  yake na  kugoma  kumsindikiza kwa madai  kuwa  yeye ni binti  na huyo ni mwanaume  iweje aombe  kusindikizwa .



 Kutokana na  mbinu  zote  kugonga  mwamba  ndipo  fundi  fataki  huyo alipoamua kutumia njia  ya mkato  ya  kumkamata kwa nguvu  binti  huyo na kutaka  kumbaka  chooni  kabla ya binti  huyo kuamua  kupambana na kuishia  kuchaniwa  sketi yake .

Hali  hiyo  ilimfanya  binti huyo kutimua mbio na kuomba msaada kwa mama  yake aliyekuwa amelala  chumba cha  pili kabla ya mama mzazi na  majirani  kuamka na  kumwadabisha  fundi fataki kwa  kumpeleka  polisi.

Hakimu  Masua  alisema  kuwa kutokana na ushahidi  uliotolewa  fundi huyo alipotakiwa  kujitetea  alikana  kujitetea kwa madai  kuwa hawezi kuzungumza chochote katika mahakama  hiyo.

Hivyo  alisema  kutokana  na  mtuhumiwa  huyo  kutenda kosa  hilo kwa mara ya kwanza mahakama  hiyo  ilipaswa  kumfunga  jela kwa miaka  mitano  kutokana na  kosa  hilo la shambulio la aibu  kifungu  cha 135 kanuni ya adhabu  namba 6 marejeo    mwaka 2002.

“ Mahakama  hii  inakuona na  hatia  na  hivyo  inakupunguzia  adhabu  kutoka miaka  mitano  uliopaswa  kutumikia na kufungwa mwaka mmoja jela  na  ukitoka  utatakiwa  kumlipa  mlalamikaji kiasi cha  Tsh 200,000”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. mimi nilitaka kushangaa! huyu bwana kesi angeishinda kiulaini kama majirani na watoto wasigetoa ushanidi.

    Ha hapa si inaonekana ? Kifungo cha miaka mitano jela kadiri ya sheria kimekuwa mwaka mmoja..HAHAHAHAHAHA. Kesi za ugakaji tz hazipo , mara zote mbakaji hushinda labda hakimu awe mwanamke. Huyu hakimu bila woga eyo mwaka mmoja badalal ya mitano.

    Wanaume kubaka naona wao huona ni haki yao.

    Lakini cha pili kwa nini huyu mama anamtega huyu bwana kumba kazi ya kulinda watoto akiwemo wa kike?

    ReplyDelete
  2. Fisi unamkabidhi bucha la nyama akulindie. Huku si kutafutana lawama jamani.

    Hapa hakimu kweli alitumia busara kumpunguzia adhabu. Siku hizi mwanafunzi wa darasa la tano; anakuwa ameshaanza kutamanisha; watoto wananona wakiwa wadogo siku hizi.

    Kwa hiyo sisi vijana kujilina na vifungo inabidi tuwe makini sana. Tusikubali kufanya kazi kama hiyo ya fisi kukabidhiwa bucha la nyama alinde.

    ReplyDelete
  3. Mwandishi wa habari hii hajali haki ya mtoto. kuomba penzi kwa mtoto wa miaka 11? hii ni lugha gani? Ndio maana ubakaji hauta isha kama hata uandishi wa habari wenyewe ndio huu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...