Na Francis Godwin Blog
FUNDI magari mkazi wa kijiweni katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bw Abdul Husein (31) amejikuta akitupwa jela mwaka mmoja na faini ya shilingi 200,000 baada kutiwa hatiani na mahakama ya mwanzo bomani kwa kosa la kutaka penzi la nguvu kwa mwanafunzi wa darasa la tano .
Fundi huyo ambaye anadaiwa kukaribishwa katika nyumba hiyo kama mlinzi wa watoto wawili akiwemo mwanafunzi huyo wa miaka 11 alitenda kosa hilotarehe 4 mwezi huu majira ya saa 3 usiku baada ya kurejea kutoka katika shughuli zake.
Akisoma hukumu hiyo leo hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo bomani mheshimiwa Alois Masua alisema kuwa katika ushahidi ambao ulitolewa mahakamani hapo na mtoto wa kiume wa miaka 9 ulidai kuwa kijana huyo siku ya tukio baada ya kufika nyumbani alimtaka binti huyo kumpa sahani ili aweke chips ambazo alikuja nazo .
Kuwa baada ya binti huyo jina limehifadhiwa na mtandao huu kumpa sahani ndani ya dakika chache aliomba kupewa maji na binti huyo alifanya hivyo baada ya kupewa maji kijana huyo alimtaka binti huyo kusogea kukaa katika eneo kochi ambalo fundi huyo amekuwa akilitumia kama kitanda chake sebuleni kama mlizi bado binti huyo aligoma kuingia majaribuni .
Hata hivyo haikuishia hapo baada ya muda fundi huyo fataki alimtaka binti huyo kumsindikiza chooni bado binti alionyesha msimamo wa kutamani masomo yake na kugoma kumsindikiza kwa madai kuwa yeye ni binti na huyo ni mwanaume iweje aombe kusindikizwa .
Kutokana na mbinu zote kugonga mwamba ndipo fundi fataki huyo alipoamua kutumia njia ya mkato ya kumkamata kwa nguvu binti huyo na kutaka kumbaka chooni kabla ya binti huyo kuamua kupambana na kuishia kuchaniwa sketi yake .
Hali hiyo ilimfanya binti huyo kutimua mbio na kuomba msaada kwa mama yake aliyekuwa amelala chumba cha pili kabla ya mama mzazi na majirani kuamka na kumwadabisha fundi fataki kwa kumpeleka polisi.
Hakimu Masua alisema kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa fundi huyo alipotakiwa kujitetea alikana kujitetea kwa madai kuwa hawezi kuzungumza chochote katika mahakama hiyo.
Hivyo alisema kutokana na mtuhumiwa huyo kutenda kosa hilo kwa mara ya kwanza mahakama hiyo ilipaswa kumfunga jela kwa miaka mitano kutokana na kosa hilo la shambulio la aibu kifungu cha 135 kanuni ya adhabu namba 6 marejeo mwaka 2002.
“ Mahakama hii inakuona na hatia na hivyo inakupunguzia adhabu kutoka miaka mitano uliopaswa kutumikia na kufungwa mwaka mmoja jela na ukitoka utatakiwa kumlipa mlalamikaji kiasi cha Tsh 200,000”
mimi nilitaka kushangaa! huyu bwana kesi angeishinda kiulaini kama majirani na watoto wasigetoa ushanidi.
ReplyDeleteHa hapa si inaonekana ? Kifungo cha miaka mitano jela kadiri ya sheria kimekuwa mwaka mmoja..HAHAHAHAHAHA. Kesi za ugakaji tz hazipo , mara zote mbakaji hushinda labda hakimu awe mwanamke. Huyu hakimu bila woga eyo mwaka mmoja badalal ya mitano.
Wanaume kubaka naona wao huona ni haki yao.
Lakini cha pili kwa nini huyu mama anamtega huyu bwana kumba kazi ya kulinda watoto akiwemo wa kike?
Fisi unamkabidhi bucha la nyama akulindie. Huku si kutafutana lawama jamani.
ReplyDeleteHapa hakimu kweli alitumia busara kumpunguzia adhabu. Siku hizi mwanafunzi wa darasa la tano; anakuwa ameshaanza kutamanisha; watoto wananona wakiwa wadogo siku hizi.
Kwa hiyo sisi vijana kujilina na vifungo inabidi tuwe makini sana. Tusikubali kufanya kazi kama hiyo ya fisi kukabidhiwa bucha la nyama alinde.
Mwandishi wa habari hii hajali haki ya mtoto. kuomba penzi kwa mtoto wa miaka 11? hii ni lugha gani? Ndio maana ubakaji hauta isha kama hata uandishi wa habari wenyewe ndio huu!
ReplyDelete