Ankal hebu wastue hawa jamaa wa manispaa ya Ilala waache utani na kazi na wawe waungwana kwa kuwajibika ipaswavyo katika matumizi ya hela zetu za kodi. Mwanzoni mwa juma nilipita maeneo haya ya Ocean Road jijini Dar na kukuta wamemwaga udongo katika shimo lililodumu hapo kwa takriban mwaka mmoja. Udongo wa mfinyanzi kama picha ya juu inavyoonesha, halafu haoooo wakaondoka zao. Ishukuriwe mvua haikunyesha...maana pangebakia tope tupu hapa...
Siku tatu baadaye jamaa hao wakiwa kama 12 hivi wakaja na kigari chao na kunyunyiza takriban kopo moja la lami juu ya huo udongo wa mfinyanzi na kumwagia mchanga juu yake. Kisha haoooo wakaondoka zao. Hadi leo nimepita tena hali ni hiyo hiyo. Mimi si mhandisi lakini sidhani kama hii ni njia sahihi ya kuziba mashimo kibao yaliyotapakaa jiji zima. Kama kashimo kamoja kanachukua mwezi kuzibwa na wafanyakazi kibao, je itachukua muda gani kumaliza kuziba mashimo yote jijini?
Mdau Muungwana
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...