Kanali Sam Kirya kushoto na Brigedia
Jenerali Michael Ondoga wakiwa kizimbani
Na Swahili TV
Kamanda wa wa zamani wa jeshi Uganda la kulinda amani  nchini Somalia (AMISOM) , Brigedia Jenerali Michael Ondoga, na wenzake wawili ameshitakiwa kwa tuhuma za kuiba na kuuza chakula na mafuta ya wanajeshi wanaotumika katika nchi hiyo. Pia jenerali huyo ameshitakiwa  kwa mashitaka mengine nane  yanayohusiana na utendaji wake.
Akisimama mbele ya mwenyekiti wa mahakama ya kijeshi Brigedia Moses Ddiba Ssentongo, Jenerali Ondoga alisomewa mashitaka yake na mwendesha mashitaka kuwa Jenerali Ondoga anatuhumiwa mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, huku akijua  jukumu la kijeshi katika eneo la Afgooye-Baidoa kwa makusudi alipeleka wanajeshi 1000 badala ya 1500 na hivyo kusababisha vifo vya wanajeshi pia alishindwa kutoa maelekezo kwa kamanda wa kundi X kitendo kilichosababisha upotevu wa kifaru na wanajeshi wake.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Jenerali Ondoga anatuhumiwa pia kushindwa majukumu yake Oktoba mwaka jana pale  aliposhindwa kushughulikia upungufu wa chakula licha ya malalamiko kutoka kwa makamanda, na pia alishindwa kumudu wanajeshi walio chini yake kitendo kilichopelekea uhamisho wa Kapteni Rubahimbwa aliyekuwa akipingwa kutokana na utendaji dhaifu wa majukumu yake.
Inatuhumiwa pia kuwa  Jenerali alishindwa kuitisha bodi ya uchunguzi ili kuangalia  utoro wa Saameja wake bwana Keneth Mugusha aliyetoroka na  kutorosha lita 15,000 za mafuta kilichohatarisha mipango ya kijeshi ya kikosi chake.
Jenerali Ondoga pia anashitakiwa kuingilia upelelezi kwa kuchukua nyaraka zinazohusiana na uchunguzi na pia kuwadhalilisha walio chini    yake kuhusiana na kuwekwa kizuizini kwa Saameja Coleb Kashumbusha kwa siku saba.
Katika mashitka mengine, Jenerali Ondoga ameunganishwa katika mashitaka na Luteni kanali Sam Kirya ofisa habari  wa zamani wa jeshi la kulinda amani nchini Somalia, kwa kutoa habari za uongo kuhusu  mahali walipo maadui katika miji ya Janale na Sharambot, wawili hao pia wameshitakiwa kwa kushindwa kuzuia ugomvi wa madaraka katika kituo cha Aljazeera.
Hata hivyo Brigedia jenerali Ondogo na wenzake wamekanusha mashitaka, wako rumande hadi novemba 5 mwaka huu.Rais Yoweri Museveni hivi karibuni aliwarudisha nyumbani karibu  maofisa 24 wa jeshi lake akiwepo Ondoga kwa tuhuma za kuuza chakula cha wanajeshi, hatua hiyo ilifuatia uchunguzi wa kitengo cha usalama cha jeshi la Uganda kubaini wizi wa chakula, mafuta na rushwa iliyoshamili katika kikosi maalum cha kulinda amani nchini Somalia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hao ndio Maboss wa Kijeshi (Ma-Brigadier, Ma-Colonel, Ma-Major na Ma-Captain) wa mmoja wa Maraisi wa inayojiita 'The Coaliton of willing' ktk hii Afrika ya Mashariki yetu yenye mashaka mashaka!

    Hao ndio Mabosi wa Kijeshi wa 'The Coalition of the willing' !!!

    Hivi Kiongozi wa Kijeshi anaiba mali, anakula rushwa, anadanganya, anahujumu, anakiuka utendaji wake Kikazi tena akiwa ktk Operesheni za Kijeshi za Kivita!

    Kweli tutasimamia wapi Watanzania na Tanzania endapo ikitokea tukubaliane na hiyo ''The Coalition of willing'' ambayo ina Mabosi wake wa Kijeshi wapo namna hiyo?

    ReplyDelete
  2. Panauwezekano mkubwa sana ktk hayo Makosa mengine 8 ambayo hayakutajwa ya hao Maboss wa Kujeshi wa Uganda huko Somalia kuwepo ULAWITI, UNAJISI na UBAKAJI dhidi ya kundi la ki-Raia!

    ReplyDelete
  3. Ohhh makubwa!

    Hayo ni Majeshi ya Serikali ya Uganda ama Majeshi ya Waasi wa Uganda?

    Halafu inatokea ktk Afrika ya Mashariki Majeshi yanaungana na Majeshi ya Uganda yanakuja tumikia Tanzania!, kwa hali hii?

    Angalieni Majeshi yetu Maadilifu ya Tanzania yanakufa yakiwa ktk Kupigania Amani chini ya UN lakini Majeshi ya wenzetu Uganda kwa kwenda mbele ni Uhalifu vitani!

    ReplyDelete
  4. Hawa wanajeshi wa Afrika vipi uraia umewaingia sana au?

    ReplyDelete
  5. Halafu Kagame na Museveni mnataka kuharakisha Political Federation ama Umoja wa Kisiasa !

    Muelewe Umoja wa Kisiasa unajumuisha kuunganisha vitu kama:

    1.Majeshi-Military
    2.Mahakama-Law and order
    3.Mihimili ya Sheria-Justice Peace and Tranquility

    Itakuwa vipi haraka zenu wakati bado hamjayaweak Majeshi yenu kuwa na Uadilifu kwa kuitumikia jamii ya Uraiani?

    Ni wazi Majeshi yenu yangali na mtazamo ule ule wa Kimsituni mlikotokea!!!,,,ndio maana yote haya yanatokea.

    ReplyDelete
  6. Ohoooo ndio Majeshi yenu yalivyo?

    Halafu ndio nyie Uganda na Rwanda mnataka Muungano na sisi, mnataka kuharakisha Maazimio ya Muungano na sisi!!!

    ReplyDelete
  7. Hizi ndio Gharama zilizo fichika zitakazo tukuta kama tukikurupuka kusaini Maazimio ya Muungano wa Afrika ya Mashariki na nchi Wanachama zenye Majeshi ya namna hii.

    Ktk Muungano huu wa EAC patafikia Majeshi ya nchi wanachama yanaunganishwa na kutumikia nchi zote!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...