Na Abdulaziz Video,Kilwa
Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Kilwa kimekutana leo
katika kikao cha kawaida chini ya Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bw
Ally Mohamed Mtopa ambapo Madiwani wa Halmashauri hiyo wamemtaka
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Addoh Mapunda kutoa majibu ya Magari
ya Halmashauri hiyo yaliyo katika karakana mbalimbali ili wajue hatma
ya magari hayo ambayo yapo kwa muda mrefu huku shughuli za Halmashauri
zikiendelea kukwama
Kufuatia hoja hiyo,Mkurugenzi aliwaeleza madiwani hao kuwa Kamati ya
Fedha na Uchumi ilipitia kukagua magari hayo na kutoa Ushauri kwa
Halmashauri hiyo kuuza magari hayo kutokana na uchakavu ili yanunuliwe
magari mapya
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Bw Ally Mohamed Mtopa akiongoza kikao hicho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...