Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii, Moshi.
JUMLA ya wanamichezo 44 wa mchezo wa Judo kutoka katika vilabu vitano
wanachuana katika mashindano ya kwanza ya mchezo huo Kitaifa ambayo yatafanyika katika chuo cha mafunzo ya Polisi Moshi.
Mashindano hayo ambayo yanadhaminiwa na Chuo hicho yatashirikisha
vilabu vya Magereza ya Ukonga, Flamingo, Kisutu (Dar es salaam), Chuo
cha Polisi Moshi (Kilimanjaro), Korogwe (Tanga).
,
Mrakibu msaidizi wa Polisi, Hamisi Msolo amesema leo kuwa lengo la mashindano
hayo ni kupima na kupandisha viwango vya wachezaji wa Judo katika
uzito wa kilo 60, 66, 80, 90 na kilo 100 ambapo watakaoshinda
wataiwakilisha Taifa katika mashindano ya kanda ya Tano
yatakayofanyika mwakani mwezi ujao katika jiji la Nairobi nchini
Kenya.
Kwa upande wake Katibu wa chama cha Judo Taifa (TJA), Innocent Mallya
alisema mchezo wa judo kwa sasa unakuwa lakini tatizo ni udhamini
mdogo kwani serikali haijalekeza nguvu za kutosha katika mchezo huo.
Alikipongeza Chuo cha Polisi Moshi kwa kuamua kuandaa mashindano hayo
ambayo ni mara ya kwanza kuandaliwa na Klabu jambo ambalo alisema
litachangia kukuza hamasa kwa wananchi kuupenda mchezo huo.
Aidha kuhusu changamoto nyingine Mallya alisema mchezo huo ambao
unategeamea mno mafunzo na sio kipaji ni vifaa vinavyotumika vina
gharama sana jambo linalokwamisha ari ya mchezaji mmoja mmoja
kujiendeleza katika mchezo huo.
Zawadi katika Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Mkuu wa Chuo cha MPA,
Matanga Mbushi kwa kushirikiana na Marenga Investment, Ibra Line,
Tanzanite One, pamoja na Benki ya NMB tawi la Mandela ni Medali na
fedha taslimu.
Afisa michezo wa chuo cha taaluma ya Polisi ,Moshi Mkaguzi Msolo .H.Msolo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza kwa mashindano ya Judo katika chuo cha polisi leo.kulia kwake ni Mwalimu wa mchezo huo Mkaguzi Fredy Mpandula.
Washiriki wa mchezo wa Judo ambao watashiriki mashindano ya mchezo huo leo.
Washiriki wa mchezo wa Judo ambao watashiriki mashindano ya mchezo huo leo.
Makamu mwenyekiti wa chama cha mchezo wa Judo Tanzania Bw. Omary Mgowe akizungumza katika kikao hicho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...